Wednesday, May 8, 2013

MTOTO WA MIAKA 3 AKUTWA AMEKUFA MTO MOROGORO.


Mtoto mwenye umri wa miaka 3 aitwaye Issa Iddi amekutwa amekufa katika mtkondo wa mto Morogoro eneo la Mafisa karibu na Mabwawa ya majitaka yanayomilikwa na MORUWASA.Tukio hilo limetokea leo asubuhi ambapo wakulima wa mpunga wamekuta maiti ya mtoto huyo imenasa.
Maiti ya mtoto Issa Iddi aliyekutwa amekufa mto morogoro.
Bofya Read more kuendelea.

Kwa maelezo ya mama wa mtoto huyo aitwaye Merry Mkembu anayefanya kazi katika kiwanda cha nguo cha 21st Century Textiles (Polyster) anasema alienda kazini juzi usiku na kumuachia mdogo wake wa kiume  aitwaye Josiah Mkembu mtoto huyo ili akirudi amkute kesho yake (jana). Ameendelea kusema kuwa jana baada ya kutoka kazini alienda kwa mdogo wake huyo ili amchukue mwanae.Alipofika akamuuliza mdogo wake Issa yuko,mdogo wake akasema kwani hajaja huko?
Ndipo wakaanza kumtafuta na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Sina kuwa mwanake kapotea.
Mamake mtoto aitwaye Merry Mkembu watu wakimshika baada ya maiti kutolewa kwenye mto.

Mjomba wa marehemu aitwaye Josiah Mkembu aliyeachiwa mtoto.
Na kwa maelezo yake mjomba wa marehemu anasema kuwa kweli aliachiwa huyo mtoto juzi jioni na dadake ili aende kazini.Anasema baada ya kuachiwa huyo mtoto alienda kunywa pombe jirani na huyo mtoto na anasema baadae wariludi ndipo mtoto akawa anamsumbua kuwa nataka kwenda kwa mama yake.Anaendelea kueleza kuwa baada ya kumsumbua kwa muda mrefu ndipo alipomruhusu aende ili asimsumbue lakini anasema alifanya hivyo akiamini kuwa hawezi kwenda popote.
mwenyekiti wa mtaa Sina John Sweya akiwa katika eneo la tukio.
Naye  mwenyekiti wa mtaa wa Sina Ndg.John Sweya akielezea tukio hilo alisema kuwa jana alipokea taarifa ya kupotea kwa mtoto Issa Iddi kutoka kwa mama yake.Hata hivyo anasema waliendelea kumtafuta mpaka leo alipopokea taarifa za kuwa kuna maiti ya mtoto imekutwa bondeni (Mto Morogoro).
Diwani wa Kata ya Mafisa Mh.Emiry Kayenzi akiwasili eneo la tukio.
Lakini tukio hilo bado ni la sintofaamu maana watu wengi waliokuwa katika eneo la tukio walikuwa wanasema huenda ametupwa makusudi aidha baada ya kuuawa au vinginevyo maana sehemu ilikokutwa maiti na anakodaiwa kutoka ambako ni nyumba za wafanyakazi za kiwanda ni takribani kilometa 3 na watu wanasema si rahisi mtoto aende mwenyewe.
Askari polisi akiutoa mwili wa marehemu.

Mili wa marehemu ukiopolewa na askari polisi.
Baadae jeshi la polisi lilifika na kuuopoa huo mwili wa marehe na kuenda nao kituo kikuu cha polisi mjini Morogoro.


Mwili wa marehemu unavyoonekana kabla ya kuopolewa.

Umati wa watu waliofurika kushuhudia tukio hilo.


Askari polisi akiwasogeza watu kabla ya kuuopoa mwili.




Mashamba ya mpunga uliolazwa na kualibiwa vibaya na watu walifurika eneo la tukio.





Mwili ukipelekwa kwenye gari.


Askari na watu wakivuka mto






 

1 comment:

  1. Anonymous12:48 PM

    inasikitisha sana..mungu ailaze roho ya mtoto mahala pema peponi...pole kwa wazazi pia..hakika ni wakati mgumu sana

    ReplyDelete

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...