Wakati
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikitarajiwa kutoa uamuzi wa maombi
ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare leo,
pia itasikiliza rufaa ya kesi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa
wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah
Zombe.
Lwakatare
na mwenzake, Ludovick Rwezahula Joseph wanakabiliwa na kesi ya ugaidi,
walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18
na kusomewa mashtaka manne yakiwamo ya ugaidi.
Taarifa
zilizopatikana jana kutoka Mahakama Kuu na kuthibishwa na mmoja wa
mawakili wanaomtetea Lwakatare, zilisema uamuzi wa maombi hayo utatolewa
na Jaji Lawrence Kaduri leo saa 3:00 asubuhi.
Kuhusu Zombe, Mahakama Kuu itaamua ama kutupiliwa mbali, au kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.
Zombe
alikatiwa rufaa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) akipinga hukumu ya
Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake katika kesi ya mauaji ya
wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro na dereva
teksi wa Manzese, Dar es Salaam.
Chanzo:CHADEMA social media.
No comments:
Post a Comment