LEO ni Mei 21 siku ambayo Taifa
linaingia kwenye kumbukumbu chungu ya kutimia miaka 17 tangu kutokea
kwa ajari mbaya ya Mv Bukoba iliyochukua maisha ya Watanzania zaidi ya
300 waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza.
Mara
kadhaa watu wachache walionusurika katika ajari hiyo wamekuwa
wakijitokeza kutoa ushuhuda wao jinsi mambo yalivyokuwa wakati Meli
hiyo ilipopinduka ikiwa inakaribia kuingia Bandari ya Mwanza.
Kitu
cha ajabu ni kuwa mpaka leo serikali inaonekana bado iko
usingizini katika kuweka umakini kwa vyombo vya usafiri nchini jambo
linalofanya kuwepo kwa ajari za mara kwa mara zinazogharimu maisha
ya watanzania wengi kwa uzembe wa watu wachache.
Siku
za hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia ajari mbaya za barabarani na majini ambazo
zimekuwa zikiacha historia na majonzi kwenye familia mbalimbali,pia
kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Makaburi ya pamoja ya Ndugu zetu yaliyo Igoma-Mwanza. |
Hivyo ni ombi na vilio vya wananchi kwa serikali, waendeshaji vyombo vya usafiri na wadau mbalimbali wa sekta hii kuwa makini katika kudhibiti ajari zisizo za lazima kutokea....
Mwisho naomba kuwapa pole wahanga wa ajari ya MV.Bukoba na watanzania wote kwa ujumla mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwafariji.
Amina!!
Amina!!
Meli Ya MV Bukoba...ikizama Ziwa Victoria,Miaka 17 iliyopita! |
Mnara wa kumbu kumbu. |
No comments:
Post a Comment