Saturday, May 18, 2013

MABOMU YAUA 77 NA KUJERUHI KADHAA - IRAQ


Wimbi  la mashambulio ya mabomu limewaua kiasi ya watu 77 na kuwajeruhi wengine wengi nchini Iraq hapo jana huku ghasia za kimadhehebu zikiongezeka  nchini humo.

Kituo cha televisheni cha Alsumaria kimeripoti kuwa takriban watu 20 wameuawa na wengine 32 wamejeruhiwa wakati  mabomu ya kutegwa kando ya barabara yaliporipuka moja baada ya jingine katika eneo la kibiashara katika mji wa Amariya magharibi mwa mji mkuu Baghdad.

Katika mji wa Baquba bomu lililotegwa katika gari liliripuka nje ya msikiti wa Wasunni na kuwaua watu 38 na  wengine 55 wamejeruhiwa. Mripuko huo ulitokea wakati waumini walipokuwa wakitoka kusali sala ya mchana.Picha katika vituo vya televisheni nchini humo zimeonyesha miili ikiwa imetapakaa karibu na msikiti huo maarufu wa Saria.watu saba wameuwawa na wengine 10 wamejeruhiwa wakati bomu liliporipuka katika mazishi ya kaka yake mbunge wa kisunni katika eneo la Bayia magharibi mwa Baghdad.

Watu wengine 10 wameuawa na wengine 32 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu katika mazishiya kishia katika mji wa Maadan kusini mwa Baghdad.

SOURCE: DW

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...