Saturday, May 18, 2013

SHEREHE ZA UBINGWA ZANOGA, YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0



Sherehe za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa Mabingwa wapya Young Africans zimenoga baada ya mabingwa wapya kuichapa timu ya Simba SC mabao 2 -0 katika mchezo uliofanyika katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na watazamaji wapatao elfu 60 huku kituo cha luninga cha Supersport kutoka nchini Afrika Kusini kikirusha moja moja kwa mchezo huo
Young Africans ambayo ilishatwaa Ubingwa wa VPL kabla hata ya Ligi kumalizika iliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha inaiubuka na ushindi katika mchezo kitu ambacho ndicho kilichotkea kwa watoto wa Jangwani kwa kuibuka na ushindi huo.
Kikosi cha Young Africans kiliingia uwanjani kwa kuonyesha kinahitaji ushindi tangu mwanzo wa mchezo huku washambuliaji wake na nafasi ya kiungo wakiwaatesa wachezaji wa Simba  na kushindwa kuonekana kabisa.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Didier Kavumbagu alikuwa wa kwanza kuipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 4 ya mchezo kwa kiichwa akimalizika mpira uliopigwa pia na mbuyu Twite kwa kichwa kufuatia kona iliyopigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Goli la kwanza.
Baada ya bao la hilo Yanga iliendelea kulishambulia lango la Simba kupitia kwa washambuliaji wake Saimon Msuva, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza na kama si umakini wa mlinda mlango Juma Kaseja basi Yanga ingeweza kuibuka na mabao mengi zaidi.  

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans ilikua mbele kwa bao 1- 0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba ikifanya mabadiliko ili kujaribu angalau kuweza kupata bao la kusawazisha, lakini ukuta wa Yanga ulikuwa imara kitu ambacho  kiliendelea kuwapunguza  makali washambuliaji wao.
Dakika ya 63 Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao pili kufuatia mpira uliorushwa na mlinzi Mbuyu Twite kugusa kwa kichwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' kabla ya kumkuta Hamis Kiiza aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la pili.
Nizar Khalfani aliyechukua nafasi ya Hamis Kiiza nusura aipatie Yanga bao la tatu dakika ya 88 ya mchezo baada ya mpira wa adhabu alioupiga kuokolewa na mlinda mlango Juma Kaseja ambaye ilibidi atibiwe kwa dakika kadhaa kufuatia kupata maumivu.
Dakika ya 89 ya mchezo mwamuzi Martin Saanya ilibidi atibiwe kufuatia kuishiwa nguvu ghafla wakati akiamulia kutokuelewana kwa wachezaji Nassoro Masoud 'Chollo' na Didider Kavumbagu, huduma ya kwanza na madaktari walimpa msaada akaamka kisha kuendelea na pambano.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC.
Kikosi cha Yanga: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (c), 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd 'Chuji' 7.Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu, 10.Hamis Kiiza/Nizar Khalfani, 11.Haruna Niyonzima
Simba : 1.Juma Kaseja, 2.Nassoro Msoud, 3.Haruna Shamte, 4.Mussa Mudde, 5.Shomari Kapombe, 6.Wlilliam Lucian, 7.Mwinyi Kazimoto, 8.Abdallah Sesseme, 9.Mrisho Ngassa, 10.Amri Kiemba/Jonas Mkude, 11.Haruna Chanongo/Abdallah Singano




No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...