Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Thursday, February 13, 2020

MKUTANO WA KWANZA WA KAMATI YA MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MENEJIMENTI YA MAAFA KWA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira,  Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.
Ndugu Wananchi,
Serikali ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.

Tuesday, April 14, 2015

Al Shabaab waua watu 9 katika majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.

Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo

kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.

Wednesday, November 19, 2014

Bill Gates kusaidia kupambana na Ebola.

Mfuko wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio.
Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi.
Mpaka sasa hakuna dawa iliyoidhinishwa wala chanjo ya kupambana na Virusi vya Ebola,matibabu ya hospitalini hutolewa kwa kuwapa wagonjwa maji ili kufunga kuharisha na dawa za kupambana na vijidudu.
Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake na namna zinavyofanya kazi.
Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF linatarajia kuanzisha majaribio ya tiba Afrika Magharibi mwezi Desemba.
Mfuko huo unamilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates na mkewe Melinda umesema kuwa utafanya kazi na washirika kadhaa kwa ajili ya kutengeneza tiba.
Tiba hiyo itatumia damu iliyotolewa na watu waliopona maradhi ya Ebola.
Akiongea mwanzoni mwa mwezi huu, Bill Gates alisema utafiti zaidi kuhusu Ebola unahitajika .

Chanzo: BBC

Thursday, September 25, 2014

Wafuasi wa Boko Haram wajisalimisha.

Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram akijidai kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo, Abubakar Shekau.

Friday, September 19, 2014

55% YA SCOTLAND WAKATAA KUJITENGA KUTOKA UINGEREZA.

Scotland imefanya uamuzi wa mwisho kuwa itaendelea kubaki sehemu ya Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland.
Maeneo 31 kati ya 32 wamepiga kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura 1,914,187 dhidi ya 1,539,920.
Ushindi huo ni asilimia 55 dhidi ya 45 waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.
Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.
Chanzo:BBC

Friday, September 12, 2014

Oscar Pistorius hatiani kwa kuua bila kukusudia.

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya
Akitoa uamuzi wake Jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp nw akutekeleza mauaji hayo kwa kusudi.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Chanzo:BBC

Thursday, September 11, 2014

Pistorius hakukusudia kuua - Mahakama yasema

Pistorius amekana kumuua mpenzi wake kwa maksudi
Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.

Wednesday, August 6, 2014

Mshukiwa wa Al shabaab akamatwa Kenya

Wapiganaji wa Al Shabaab
Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema wamemnasa mshukiwa mkuu wa Al-Shabaab mjini Nairobi. Mshukiwa huyo alikuwa nchini Kenya kutafuta matibabu.
Duru zingine zinasema kuwa alikuwa mwanahabari zamani na anashukuwa kujihuhusisha na mauaji ya waandishi wa habari wa Somali huko Mogadishu.

Monday, July 28, 2014

Ukrain kujibu mapigo

Wanajeshi wa Ukrain
Jeshi la Ukrain limeanza kujihami mashariki mwa nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Urusi kufuatia kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia katika eneo hilo.
Msemaji wa serikali ya Ukrain Andriy Lysenko amesema jeshi la nchi hiyo lilidhamiria kulifunga eneo hilo ili kupisha uchunguzi wa watalaamu kuhusiana na chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.
Ndege ya Malaysia iliyokuwa imebeba watu 300 iliangushwa katika eneo hilo lililo chini ya udhibiti wa waasi.
Waangalizi wa kimataifa wanasema mapigano hayo yataadhiri uchunguzi wa ajali hiyo ya ndege, mapigano makali yameripotiwa katika amaeneo yanayozunguka mji wa Horlivka na Shakhtarsk.

SOURCE : BBC

Kombora lalipua matenki ya mafuta - Libya

Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.
Source: BBC

Monday, May 12, 2014

Boko Haramu: Waonesha wasichana waliotekwa.


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara

Chanzo: BBC

Monday, May 5, 2014

MKE WA RAIS NIGERIA ATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WA MAANDAMANO.

Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi habari zinasema.

Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Inasemekana Mke wa Rais Jonathan anahisi mama za wasichana waliotekwa walimtuma mwanaharakati huyo ili aweze kuwawakilisha.
Mchambuzi wa masuala ya Nigeria anasema Mke wa Rais Jonathan ni Mwanasiasa mwenye nguvu nchini Nigeria.
Mama Mutah mwakilishi wa jamii ya Chibok eneo wasichana hao walipotekwa wakiwa shuleni zaidi wiki mbili zilizopita, wiki iliyopita aliandaa maandamano katika mji mkuu wa Abuja.
Waandamanaji wengi wakiwa ni Wanaigeria wanaona serikali haijafanya vya kutosha kuwatafuta wasichana hao waliotekwa wanaodhaniwa kuwa ni kundi la kiislam la Boko Haram.

Hadi sasa Boko haram hawajasema lolote kuhusu tuhuma hizo.
Wasichana wanne walio mbele ambao ni miongoni mwa waliotekwa na kufanikiwa kutoroka.


Chanzo: BBC

Thursday, April 17, 2014

Updates: AJALI YA MELI KOREA KUSINI, 179 WAOKOLEWA.

Watu 179 waokolewa mpaka sasa huku karibu watu 300 hawajulikani walipo baada ya meli iliyobeba abiria 470 kuzama jana. Maofisa wasema watu 9 wamepoteza maisha mpaka sasa.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea blogu hii.

Wednesday, April 16, 2014

Updates: WALIONUSURIKA KATIKA MELI ILIYOZAMA KOREA WASIMULIA.

Meli ya Korea Kusini ikizama
Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha."watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460.
Chanzo: BBC

Breaking news: MELI YAZAMA

Meli yenye abiria 450 wengi wao wakiwa wanafunzi imezama karibu n Pwani ya Korea Kusini usiku wa kuamkia leo. Watu 56 wameokolewa mpaka sasa.
Kwa habari zaidi juu ya tukio hili endelea kutembelea blogu hii.

Tuesday, April 15, 2014

Mke wa Rais wa Kenya aweka historia London, akimbia mbio za Marathon.


Mama Margaret Kenyatta mke wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amekuwa mwanamke wa kwanza mama wa taifa kushiriki mbio za London Marathon na kumaliza mbio hizo.
Alishangiliwa na wakenya wanaoishi nchini Uingereza alipomaliza mbio hizo za kilomita 42 kwa muda wa saa saba na dakika nne siku ya Jumapili.
Bi Kenyatta akilakiwa na mumewe Rais Uhuru Kenyatta

Bi Kenyatta alishiriki mbio za London Marathon kama sehemu ya mradi wake wa kuchangisha pesa za kuwasaidia wanawake wajawazito kujifungua katika mazingira salama na kuhakikisha kuwa watoto wao pia wanaishi nchini Kenya.Mama Margaret alilakiwa na Rais Kenyatta pamoja na waandalizi wa mbio hizo mjini London mwishoni mwa mbio huku akiwapa motisha wakenya na jamii ya kimataifa kwa kuwa mke wa kwanza wa rais kuwahi kushiriki mbio hizo.
Lengo lake kuu ni kupunguza idadi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Wanawake wengi na watoto wachanga nchini Kenya hupoteza maisha yao wakati wa kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma salama na sasa mama Kenyatta amejitwika jukumu la kuwapa akina mama wajawazito uwezo wa kujifungua salama.
Bi Kenyatta alikuwa na kikundi cha wasaidizi 8 waliokuwa naye hadi alipofika mwishoni mwa mbio hizo.
Wakenya kutoka sehemu mbali mbali uingereza walifika mjini London kushuhudia Bi Kenyatta akikamilisha mbio hizo.
Wakenya ndio walioshinda mbio hizo upande wa wanawake na wanaume.
Wilson Kipsang aling'aa upande wa wanaume kwa kuweka rekodi mpya ya saa mbili na dakika nne. Kipsang alifuatiwa na mkenya mwenzake Stanley Biwott.
Kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat alishikilia nafasi ya kwanza akifuatiwa na mkenya mwenzake Florence Kiplagat

Chanzo : BBC

Tuesday, March 4, 2014

Waislam walaani kuchanwa kwa Koran Mauritania


Mamia ya waislam wamefanya maandamano katika mji mkuu wa wa Mauritania Nouakchott, baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Koran imechanwa msikitini.
Imam ameripoti kuwa watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao waliingia msikitini , wakachana nakala za Koran na kuzitupa chooni.

Mauritania ni taifa la kiislam , likiwa na idadi ndogo ya wakristo.Polisi walifyatua mabomu ya kutolea machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa na jazba, na mtu mmoja aliuawa, duru za polisi zilieleza.
Imekuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika kampeni dhidi ya al-Qaeda na makundi mengine ya wanamgambo yanayoendesha harakati katika kanda hiyo .
Mwandishi wa habari Hamdi Mohamed El Hacen aliyeko mjini Nouakchott anasema waandamanaji walichoma vizuizi na maduka mengi na masoko yalifungwa jana siku nzima.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika kati kati mwa mji mkuu na nje ya msikiti wakipaza sauti "Mungu ni mkuu" wakidai wahusika wakamatwe na kuhukumiwa kifo kwa madai ya kukufuru uislam, alisema.

Source: BBC

Monday, February 17, 2014

MAREKANI YAMUONYA MUSEVENI WA UGANDA.

Wapenzi wa jinsia moja wanaishi maisha ya kujificha nchini Uganda.

Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...