Wednesday, May 8, 2013

MAHAKAMA KUU IMEFUTA KESI YA UGAIDI KWA LWAKATARE.

Mwandishi wa blogu hii ameripoti kutoka mahakama kuu kuwa, leo Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
 
Kwa taarifa hiyo kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
 
Taarifa zaidi zinasema kuwa ilikuwa ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
 
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...