Thursday, August 20, 2015

CHADEMA YAZUIWA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA.

POSTED THURSDAY, AUGUST 20, 2015 | BY- JULIUS MATHIAS
Serikali imekataa ombi la Chadema la kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kampeni zake Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Serikali imekataa ombi la Chadema la kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kampeni zake za uchaguzi, ikisema mazingira yaliyopo sasa hayaruhusu eneo hilo kutumika kwa shughuli za kisiasa. Serikali imetangaza uamuzi huo ikiwa ni siku tatu kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani kwa ajili ya Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25. Juzi, kwenye mitandao ya jamii kulienea habari kuwa Chadema, ambayo mgombea wake wa urais, Edward Lowassa amekuwa akivuta maelfu ya watu kwenye mikutano yake, imepanga kutumia uwanja huo unaoweza kuchukua watu 60,000 waliokaa kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zake Agosti 22. Hata hivyo, Chadema imeshakanusha taarifa kuwa itazindua kampeni zake Agosti 22. Akizungumza na vyombo vya habari jijini jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Assah Mwambene alisema Serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kuutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kwamba hakuna chama kitakachoruhusiwa kufanya hivyo. “Tulipata barua ya Chadema kuomba kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuzindua kampeni zao, tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa uwanja ule hauwezi kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa,” alisema Mwambene. Alieleza kuwa Serikali imeamua kwamba uwanja huo uendelee kutumika kwa shughuli za kimichezo ili kuepuka mihemko na athari yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa. “Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza,” alisema Mwambene. Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kilichofanywa na Serikali hakijaathiri chochote kwenye maandalizi ya harakati za chama hicho kufanya uzinduzi wa kishindo ili kukidhi matarajio ya Watanzania wanaokiunga mkono. Alisema kilichotangazwa na Mwambene kimetokana na uelewa mdogo wa masuala ya demokrasia na masuala makubwa yenye mvuto wa kitaifa na kufafanua kuwa viwanja hivyo hutumika sehemu nyingi duniani kwa kuwa kampeni ni sehemu pekee ambayo wananchi wanapata nafasi ya kuwahoji wagombea kabla hawajawapa ridhaa ya kuwatumikia. “Mwambene haelewi anachokisema. Anatumika kufunika aibu ya CCM ambayo imeona mvuto wake unaendelea kushuka kila siku. Hivyo hawana uhakika wa kujaza wafuasi kwenye eneo kubwa kama lile,” alisema. “Kwa sasa ni Chadema pekee ndiyo inayoweza kuutumia uwanja ule, ndiyo maana CCM wamekimbilia viwanja vya Jangwani ambavyo kwa sasa ni vidogo kutokana na ujenzi wa vibanda vya biashara uliofanyika,” alisema Makene. Alieleza kuwa CCM inatishwa na wingi wa watu wanaojitokeza kuiunga mkono Chadema baada ya kujionea maelfu ya watu wanaoambatana na mgombea wake wa urais hasa kwa kipindi cha kuomba udhamini mikoani. “Tumekuwa tukiambatana na watu wengi sana ambao wamejitolea kuungana nasi kila tunapokwenda. Tunajipanga kufanya uzinduzi mkubwa eneo jingine na hii inaweza isifanyike Agosti 22, kila chama kinaweza kikaanza siku kinachoona inafaa kwake,” alisema.

KUITWA KAZINI - UTUMISHI.

Wednesday, August 19, 2015

CHADEMA YATANGAZA WAGOMBEA UBUNGE 2015.

POSTED WEDNESDAY, AUGUST 19, 2015 | BY- MWANANCHI.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza majina ya wagombea ubunge katika majimbo Mgombea ubunge Jimbo la Mbarali kwa tiketi ya Chadema, Liberatus Mwang’ombe akiwaonyesha wafuasi wake, bahasha yenye fomu ya kugombea kiti hicho baada ya kuzichukua katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali, Mbeya jana. Picha na Godfrey Kahango Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza majina ya wagombea ubunge katika majimbo 135 yaliyoteuliwa na Kamati Kuu yakiwamo ya wabunge na makada wa CCM waliohamia katika chama hicho. Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Bara, John Mnyika iliorodhesha majina ya wagombea wote na majimbo yao isipokuwa 12 ambayo hayajafikiwa maafikiano ndani ya Ukawa. Katika orodha hiyo wamo baadhi ya waliokuwa wabunge na makada wa CCM, Ester Bulaya aliyeteuliwa kugombea Bunda Mjini, James Lembeli (Kahama Mjini) na Said Nkumba (Sikonge). Pia, katika orodha hiyo ambayo imechapishwa katika Ukurasa wa 35 wa gazeti hili, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole ameteuliwa kugombea ubunge jimbo la Longido kwa tiketi ya Chadema. Vilevile, kada wa Chadema, Fred Mpendazoe ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, atagombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema baada ya kulikimbia Jimbo la Segerea alilogombea mwaka 2010 na kuangushwa na Dk Makongoro Mahanga ambaye naye amejiunga na Chadema hivi karibuni. Orodha hiyo pia inajumuisha jina la Naibu Waziri wa zamani wa Kilimo, Njelu Kasaka aliyehamia Chadema, kugombea katika jimbo la Lupa. Baadhi ya wagombea ambao walishindwa kwenye kura za maoni na kurudishwa na Kamati Kuu ni pamoja na Mwita Waitara (Ukonga) na Ansbert Ngurumo (Muleba Kaskazini). Mgawanyo wa majimbo balaa Wakati huohuo; mgawanyo ya majimbo chini ya Ukawa na uamuzi wa Chadema kuwarejesha baadhi ya wagombea ubunge walioshindwa katika kura ya maoni ulizua sintofahamu katika maeneo kadhaa. Hali hiyo siku moja baada ya Ukawa kutangaza mgawanyo wa majimbo na Chadema kupata 138, CUF 99, NCCR 14 na NLD matatu. Pamoja na mgawanyo huo ulioelezwa kufanyika baada ya kuafikiana, hali ya sintofahamu iliibuka katika jimbo la Mbarali mkoani Mbeya baada ya makada wa Chadema na CUF kuchukua fomu za kugombea ubunge, kinyume na uamuzi wa kusimamisha mgombea mmoja. Maeneo mengine yanayotajwa kuwa na mvutano mkali kuhusu mgawanyo wa majimbo ni Solwa, Singida Mjini, Kilombero na Kibaha. “Kuna baadhi ya majimbo makada wa Chadema wamekilalamikia chama hicho wakidai kuwa kina nguvu zaidi, hivyo kitendo cha kuachia majimbo hayo kupewa vyama vingine vinavyounda Ukawa ni sawa na kuyapoteza kwa sababu ya vyama hivyo kutokuwa na mtandao na kuwa na wagombea wasio na nguvu,” kilieleza chanzo cha habari hizo. Hata hivyo, chanzo hicho kilisema majadiliano yalikuwa yanafanyika. Mbarali Katika Jimbo la Mbarali, mgombea wa Chadema Liberatus Mwang’ombe alichukua fomu za ubunge katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi na kuungana na Gamdusti Juma Haji (CUF) aliyechukua fomu hizo Agosti 15. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wenyeviti wa wilaya wa vyama hivyo, walisema kila chama kimefikia uamuzi huo baada ya kutokubaliana kuachiana jimbo hilo. Mwenyekiti wa Chadema Mbarali, Peter Mwashiti alisema walifikia uamuzi wa kumruhusu Mwang’ombe kuchukua fomu hiyo kutokana na kushindwa kuelewana baina yao na wenzao wa CUF. Alisema awali walipewa taarifa kwamba kamati kuu ya Ukawa iliamua jimbo hilo lichukuliwe na CUF lakini wao (Chadema wilaya) wakapeleka vielelezo kwamba mgombea aliyependezwa na CUF pamoja na chama chenyewe hawana nguvu ya kushindana na CCM. “Wakati tunaendelea na vikao vyetu, tukasikia mgombea wa CUF amechukua fomu, hivyo na sisi tumeamua mgombea wetu akachukue fomu wakati tunaendelea na vikao,” alisema Mwashiti. Mwenyekiti wa CUF wa wilaya hiyo, Bob Magagula alisema walifikia uamuzi huo baada ya kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa viongozi wa vyama hivyo ngazi ya wilaya. “Chadema hawamuamini kabisa mgombea wetu, wakati sisi CUF tunamkubali… na sababu kubwa eti mgombea wetu anatumika na mgombea wa CCM kwa vile tu ni ndugu japo kuna ukweli kwamba hawa jamaa ni ndugu lakini hii si sababu ya kumkataa,” alisema. Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro, wanachama watatu wa Chadema akiwamo Katibu wa Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema jana walijeruhiwa baada kupigwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho katika mzozo wa kurudiwa kura za maoni Katika vurugu hizo zilizotokea jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu anadaiwa kuchomoa bastola yake kabla ya kuzuiwa na ofisa usalama wa Chadema, Allan Bujo.

COMMONWEALTH SCHOLARSHIPS TENABLE IN SOUTH AFRICA: 2016 AWARDS.

Applications are invited from qualified Tanzanians for Masters and Doctorate programmes under the Commonwealth Scholarships and Fellowship Plan (CSFP).

QUALIFICATIONS
Applicants should meet all entry requirements which are found under University of choice together with language requirements. 

MODE OF APPLICATION
  • Completely filled forms should be sent directly to: commonwealthscholarships@dhet.gov.za
  • Deadline for submission of application forms not later than is 7th September, 2015.
  • Tanzanian applicants are advised to send a printed copy of completely filled application form to the Country Agency through the following address:-

The Permanent Secretary,
Ministry of Education and Vocational Training,
7 Magogoni Street,
Post Code 11479,
P. O. Box 9121,
DAR ES SALAAM

KUITWA KWENYE USAILI-TPDC.

Job Advert - EWURA.

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES - DUCE.

CALL FOR ORAL INTERVIEW - BOT.

JOB VACANCIES - TANZANIA POSTAL BANK.


JOB VACANCIES - EASTEC & ADEM.

Saturday, August 8, 2015

Ligi kuu Uingereza, Manchester United 1- Totternham Hotspers 0

Ligi kuu nchini Uingereza imeanza rasmi Leo kwa mchezo wa ufunguzi ulio wakutanisha Manchester United na Tottenham Hotspers katika uwanja was Oldtraford. Man U wameweza kuanza vizuri kwa kutoka kifua mbele kwa goli 1-0 bao lklilopatikana mnamo dakika ya 22 baada ya Kyle Walker kujifunga.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...