Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Tuesday, February 7, 2017
Wednesday, December 17, 2014
WAKURUGENZI 6 WAFUKUZWA KAZI KWA KUBORONGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, AISHA MADINDA AFARIKI.
WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia |
WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia leo amewavua madaraka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliua, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda kufuatia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba, 14 mwaka huu. Wakurugenzi wengine watano (5) bado wanachunguzwa.
Aidha Waziri Ghasia amesema kuwa hawezi kujiuzulu kama alivyoahidi baada ya watendaji waliozembea kugundulika.Kifo cha Madinda.
Msanii mnenguaji wa bendi ya Extra Bongo, Aisha Mbegu "Madinda" amefariki leo mchana katika Hospitali ya Mwananyamala na chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika.
Kwa taarifa zaidi, endelea kutembelea blogu hii.
Tuesday, November 18, 2014
Monday, September 15, 2014
UCHAGUZI CHADEMA, MH FREEMAN AIKAEL MBOWE ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI TAIFA .
MATOKEO YA UCHAGUZI
MWENYEKITI
Mh Freeman Mbowe amepata kura 789
Mh Gambaranyere Mwangateka amepata kura 20
MAKAMU BARA
Prof Abdallah Safari amepata kura 775
Hakuwa na Mpinzani
MAKAMU ZANZIBAR
Mh Said Issa Mohamed amepata kura 645
Mh Hamad Yusuph amepata kura 163
Tuesday, August 5, 2014
MCHAKATO WA KATIBA MPYA: WARIOBA,KABUDI,BUTIKU WAWASHA MOTO UPYA.
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba, uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi |
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Thursday, July 17, 2014
Wednesday, May 14, 2014
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. MCH. PETER SIMON MSIGWA, (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015.
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Frank Herbert aliwahi kusema
“Utawala bora, kamwe hautegemei Sheria bali sifa binafsi za wale wanaotawala. Vyombo vya Serikali mara zote vipo chini ya wale wanaowaongoza. Kwa hiyo sifa muhimu ya Serikali ni namna ya kuteua/kuchagua viongozi”
Serikali ya awamu ya nne, imeshindwa kuwajenga viongozi wake katika misingi bora na ndio maana pamoja na matatizo ya kimfumo, wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kubadilisha viongozi na matokeo ya ufanisi wake yamekua ni kioja na dhihaka katika utendaji.
2.0 UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO 16 YA BUNGE
Mheshimiwa Spika, kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilileta Bungeni taarifa yake tarehe 20 Disemba 2013 liyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Mhe. James Lembeli kuhusu uchunguzi wa matatizo katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyokua na maazimio kumi na sita (16). Taarifa hiyo ndiyo iliyomuondoa aliyekua Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na mawaziri wengine.
Tuesday, May 6, 2014
CUF WASEMA WASIOTAKA SERIKALI YA UMOJA WAFUKUZWE.
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin kusema kuwa Wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa au vinginevyo.
Salmin aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja kwa kuwa wanaona kwamba lengo la kuundwa kwake halina dalili njema kwa siku za usoni.
Thursday, April 17, 2014
JUKWAA LA KATIBA LA LAANI KAULI ZA LUKUVI ALIZOTOA BUNGENI
Mchana huu jukwaa la katiba limetoa tamko kulaani kauli alizotoa Waziri William Lukuvi Jumamosi kuhusu jeshi kuchukua nchi kama serikali 3 zikiridhiwa.
Hata hivo, leo tena Waziri Lukuvi akiongea Mjini Dodoma ameonesha hofu yake juu ya udini. ." Uamsho ni taasisi ya kidini inayotekeleza sera za kisiasa za CUF, latia hofu kuibuka chokochoko za kidini nchini" asema Lukuvi.
Monday, April 14, 2014
ALICHOSEMA ZITTO KABWE JUU YA SERIKALI 2 AU 3.
Kuna ambao wanaamini kabisa kwamba kuifukua Tanganyika ndani ya Muungano kutavunja Muungano na hivyo wanataka S2 ziboreshwe. Kuna ambao wanataka S2 kwa kufuata mkumbo tu na kwamba ni 'sera' ya chama chao.
Kuna ambao wanaamini kabisa kwamba S3 ndio njia ya kuimarisha Muungano na kuufanya endelevu kwa kuweka uwazi katika muundo wa Muungano na usawa wa Washirika. Kuna ambao S3 ni njia ya kutokea kuelekea kuvunja muungano maana ama hawaamini katika muungano au hawana itikadi yeyote (ideological bankruptcy).
Wanaong'ang'ania S2 wakidhani wanalinda Muungano watambue kuwa wanawapa nguvu S3 wanaotaka kuvunja muungano.
Ni busara na maono ya mbali kwamba wale wanaoupenda Muungano ( ideologically clear people) kuhakikisha S3 zenye Serikali imara ya muungano. Usipotaka mabadiliko, mabadiliko yatakutaka. Tafakari
Chanzo: Zitto social media.
Tuesday, March 25, 2014
SERIKALI YAVUNJA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012. Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.
Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.
Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Dar es Salaam.
25 Machi,2014
Wednesday, February 19, 2014
ALICHOKISEMA ZITTO KABWE SIKU YA LEO.
Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13.
Tangu gazeti dada la The Citizen lichapishe mwishoni mwa wiki habari za upotevu wa Sh480 bilioni katika Wizara ya Fedha, Serikali imekaa kimya kama vile wizi huo ni tukio la kawaida, hivyo halihitaji maelezo ya kina wala ya haraka. Wananchi walitegemea kwamba Serikali ingetoa kauli haraka iwezekanavyo kuhusu mazingira ya upotevu huo na hatua inazochukua kuwawajibisha wahusika.
Friday, February 7, 2014
KUMBE MH. ZITTO KABWE NI MWALIMU, LEO AFUNDISHA SHULE YA MSINGI MUUNGANO - UJIJI KIGOMA.
BUNGE LA KATIBA KUANZA VIKAO FEBRUARI, 18.
Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.
Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.
Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.
Bunge la Katiba linafanyika baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake ya miezi 20 kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya pili Katiba ambayo ilitolewa Desemba 30, mwaka jana.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo jana katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Rais Kikwete alisema kama wanasiasa wakikubaliana, hakuna mwananchi yeyote atakayepinga uamuzi utakaopitishwa na Bunge hilo.
“Nimeshauriana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kuwa Bunge Maalumu la Katiba lianze vikao Februari 18, mwaka huu. Bunge hili litafanyika kwa siku 70 na kama mambo yatakuwa hayajamalizika zinaweza kuongezwa siku 20,” alisema Rais Kikwete.
Tuesday, January 28, 2014
DR. REGINARLD MENGI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM KINANA
Thursday, October 17, 2013
ZITTO KABWE AVIJIBU VYAMA VYA SIASA VINAVYOMUANDAMA KUHUSU KUKAGULIWA HESABU ZAO.
Zitto Zuberi Kabwe hii leo ametoa ufafanuzi wa kile kinachoongelewa na vyama vya Siasa hapa nchini juu ya kukaguliwa mahesabu ya ruzuku kama ifuatavyo:-
"Vyama vya siasa kunishambulia sio jibu la matakwa ya kisheria ya kutaka vikaguliwe. Msajili wa vyama hana taarifa za ukaguzi. Nape anapiga kelele kuwa wamekaguliwa, anafanya siasa kwenye masuala ya kisheria. Kama anazo taarifa za ukaguzi zilizokaguliwa na CAG apeleke kwa Msajili sio kupiga kelele. Mimi nafuata sheria na kanuni za Bunge zinazotaka kusimamia matumizi ya fedha za umma. Ruzuku ni fedha za umma."
Chanzo: Zitto Social media.
Tuesday, October 15, 2013
KAULI YA ZITTO KABWE JUU YA KUTOKAGULIWA KWA HESABU ZA VYAMA VYA SIASA NCHINI.
Shilingi bilioni 67.7 zimelipwa na Serikali kwa
vyama vya siasa katika kipindi cha miaka 4, 2009/2010 mpaka 2012/2013.
Fedha hizi hazijakaguliwa kwa mujibu wa Sheria.
Mahesabu ya
Vyama vya siasa nchini yanapaswa kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Mahesabu ya Serikali kwa mujibu wa Sheria tangu mwaka 2009. Tangu
mwaka huo Kamati ya PAC haijawahi kuona Taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi wa
vyama vya siasa.
Kamati imemwita Msajili wa vyama ili kufafanua ni
kwa nini Vyama vya Siasa nchini havifuati sheria (vifungu vya sheria
vimeambatanishwa hapa chini). Uvunjifu huu wa Sheria ni wa makusudi au
wa kutokujua? Sheria inataka Mahesabu ya vyama yatangazwe kwa uwazi,
tena kwa Government Notice. Umewahi kuona? Tarehe 15 Oktoba, 2013 Kamati
ya PAC itatafuta majibu haya kutoka kwa Msajili na ikibidi vyama
vyenyewe. Tunataka uwazi wa matumizi ya Fedha za Umma.Vyama vya siasa
ndio vinaunda Serikali, uwazi unaanzia huko ili kuepuka fedha chafu kama
za EPA kuingia kuvuruga uchaguzi.
Vyama vifuatavyo vimepokea
Ruzuku ya jumla shilingi bilioni 67.7 tangu mwaka wa fedha 2009/2010;
CCM tshs 50.97 bilioni
CHADEMA tshs 9.2 bilioni
CUF tshs
6.29 bilioni
NCCR - M tshs 0.677 bilioni
UDP tshs 0.33 bilioni
TLP tshs 0.217 bilioni
APPT - M tshs 11 milioni
DP tshs 3.3
milioni
CHAUSTA tshs 2.4 milioni
Monday, October 14, 2013
YALIYOJILI KATIKA ZIARA YA ZITTO KABWE IGUNGA,NI PAMOJA NA KUTAJA KIPATO CHA RAIS.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameendelea na ziara yako Mkoani Tabora katika jimbo la Igunga Wilayani Igunga na haya ndiyo maelezo yake Zitto Kabwe juu ya kilichojili:-
"Siku ya 9 ya Ziara ya
CHADEMA kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igunga, Wilaya ya
Igunga.
Tumefanya mikutano 6 katika kata sita tofauti,
tumefungua matawi ya chama na kuhutubia wananchi. Pia tumepokea kero za
wananchi zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.
Tukiwa
Katika kata ya Choma tumeshuhudia kiwanda cha kuchambua Pamba kilicho
binafsishwa kikiwa kimetelekezwa na mwekezaji toka mwaka 1998. Ginnery
hii iliyokuwa mali ya umma na kuajiri wafanyakazi 500 kwa shifti 3 kila
siku (jumla 1500) nyakati za msimu imekufa na baadhi ya Mashine kuuzwa
kama chuma chakavu. Kijiji cha Choma kimedorora kiuchumi kutokana na
ubinafsishaji huu. Nimewaeleza wananchi kuwa nitafuatilia suala hili la
Ginnery ya Manonga, katani Choma na kuwajulisha hatua mwafaka za
kuchukua.
Sunday, October 13, 2013
Dr Slaa ahitimisha ziara Nchini Marekani.
Katibu Mkuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
,Chadema Dr Wilbroad Slaa leo Jumapili
13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania baada ya Ziara yake iliyomchukua
wiki
tatu nchini Marekani. Dr Wilbroad aliwasili nchini Marekani tarehe 21
Septemba 2013 akiambatana na Mkewe
mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV.
Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya
mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya
Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara
yake Dr Slaa alitembelea majimbo ya North Carolina na Alabama ambako
alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali na kujifunza Shughuli
nyingi za
Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na
Uchumi.
Akizungumza
akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dr Slaa alisema
alichojifunza
akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze
kumkomboa
Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni
namna
ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
Dr Slaa
amekamilisha ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la
“Vision
Tanzania” baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.Chanzo: CHADEMA Social Media
Subscribe to:
Posts (Atom)