Urusi imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuhami Syria, mara tu baada ya uamuzi wa muungano wa Ulaya wa kuondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha.
Awali, kiongozi mmoja wa waasi aliambia BBC kuwa Hezbollah imekuwa ikishambalia Syria.
Generali Selim Idriss, kwenye mahojiano na BBC alisema kuwa zaidi ya wapiganaji 7,000 wa kishia kutoka Lebanon, wanashiriki vita dhidi ya utawala wa Syria mjini Qusair, mji ambao unadhibitiwa na waasi.
Mfumo wa S-300 ni wa hali ya juu ambao unaweza kukinga makombora ya angani na ya sakafuni.
Hatua ya Urusi kuikaibidhi Syria zana kama hizo, inazua wasiwasi zaidi hasa baada ya Syria kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel, msimamo ambao pia umechukuliwa na Urusi.
Wadadisi wanasema kuwa huenda pande zinaojihusisha na mzozo wa Syria zikaanza kutumia makombora kwenye vita hivi.
Pia inahofiwa kuwa mashambulizi ya makombora yanaweza kutishia juhudi za kuandaa mkutano wa amani kuhusu Syria mjini Geneva mwezi Juni.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo sasa yamerejea katika hali nzuri ya kupambana na waasi.
No comments:
Post a Comment