TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KATIBU Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza
ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za
Mkoa wa Manyara, siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013
Katika ziara hiyo
Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja
na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara.
Akiwa katika ziara
hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo
atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili
kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na
wanachama na viongozi wa maeneo husika.
Ratiba ya ziara hiyo
itakuwa kama ifuatavyo;
Atawasili Babati
Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu
kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9
mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini.
Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang).
Tarehe 20/5/2013,
Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Haydom
(Mbulu).
Siku ya tarehe
21/5/2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh
na Mbulu Mjini.
Tarehe 22/5/2013 akiwa
njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji
vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara
Galapo, Babati Vijijini, kuanzia saa 8 mchana.
Siku ya tarehe
23/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda
na Bashnet, Babati Vijijini.
Tarehe 24/5/2013,
Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika
maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.
Siku inayofuata,
tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo
ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa
Mererani, kuanzia saa 10 jioni.
Imetolewa leo, Mei
17,2013 na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa
Habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment