|
Nigeria National Flag |
Watu waliokuwa na silaha nzito jana wamekishambulia kituo cha polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na kuwauwa watu 55, ikiwa ni pamoja na
polisi na raia. Msemaji wa jeshi Musa Sagir amesema shambulizi hilo
lilifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu katika kituo cha polisi
cha mji wa Bama, jimbo la Borno, lilisababisha vifo vya polisi 22, maafisa 14
wa gereza, wanajeshi wawili na raia wanne. Musa amesema wafuasi 13 wa
kundi hilo pia walikufa katika shambulizi hilo. Kiasi ya wafuasi 200 wa kundi la
Boko Haram waliokuwa na silaha nzito wanaripotiwa kuwasili wakiwa na
bunduki kabla ya kuushambulia mji huo. Wapiganaji hao waliokuwa na magari
aina ya pick up, kwanza waliishambulia kambi ya jeshi na kituo cha polisi
kabla ya kulivamia gereza. Hakuna kundi lililotangaza rasmi kuhusika na
shambulizi hilo, ijapokuwa jimbo la Borno ni ngome ya kundi la Boko Haram,
ambalo maafisa wanasema ndilo lililofanya shambulizi hilo.
Source: DW
No comments:
Post a Comment