Monday, April 29, 2013

WATU 19 WAUAWA IRAQ

Bendera ya Iraq.
Watu 19 wameuwa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mabomu matatu ya kutegwa kwenye gari kuripuka leo kwenye miji miwili ya Iraq, yenye wakaazi wengi wa waumini wa Kiislamu wa madhehebu ya Kishia.
Shambulio hilo limetokea kwenye miji ya Amarah na Diwaniyah, huku kukiwa na mfululizo wa ghasia za kidini kufuatia mapigano kwenye kambi ya Waislamu wa madhehebu ya Suni, kaskazini mwa Iraq.
Ghasia za kimadhehebu, zimeongezeka tangu Jumanne iliyopita, wakati vikosi vya usalama vilipojaribu kuwakamata waandamanaji katika kambi ya Waislamu wa madhdhebu ya Sunni kwenye mji wa Hawija. Hatua hiyo ilisabisha mauaji ya watu 32, wakiwemo wanajeshi watatu. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na mashambulio ya leo.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...