Tuesday, April 16, 2013

MH.MNYIKA AMLIPUA WAZIRI MKUU KUWA AMESEMA UONGO BUNGENI.


Mbunge wa Ubungo Mh.John Mnyika.
Wakati wa kufanya majumuisho na kutoa hoja,Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja mbali mbali zilizokuwa zimetolewa na Wabunge.

Wakati amemaliza kutoa hoja, Mbunge wa Ubungo CHADEMA Mh.John Mnyika aliomba mwongozo wa spika na aliporuhusiwa akaomba mwongozo kuwa Mh.Waziri Mkuu ametoa taarifa za uongo Kwanza alisema kuwa Waziri Mkuu ameliambia bunge kuwa Sheria ya kuunda mabaraza ya katiba katika ngazi ya kata ilipitishwa na bunge wakati sio kweli na pili kuwa Waziri mMkuu amesema kuwa CHADEMA hakikupeleka maoni yao ya uundwaji wa katiba mpya jambo alilolisema kuwa sio kweli na ukweli nikwamba maoni yalipelekwa na yeye mwenye wakati huo akiwa anakaimu nafasi ya Naibu katibu Mkuu.

Katika kutoa majibu,Mh.Spika alisema majibu yatatolewa kesho na kuwa muda huo hakuwa na majibu.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...