Wednesday, April 17, 2013

WATOTO 2 WAFA BAADA YA KUSOMBWA NA MAFURIKO KENYA.

 Polisi nchini Kenya wameelezea BBC kuwa watoto 2 wamekwama nyumbani kwao baada ya kufukiwa na tope na maji yaliyosababisha maporomoko ya ardhi.

Watoto hao walikuwa wamelala katika kijiji cha Narok kilomita kadhaa kutoka mji wa Nairobi, mvua kubwa iliponyesha na kusababisha maji kusomba majumba kadhaa katika mtaa wao.


Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeonya watu wanaoishi maeneo yanayotishiwa kukumbwa na mafuriko wahamie sehemu za juu na milima.

Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika sehemu nyingi nchini humo na inaaminiwa kuendelea kunyesha.

Katibu mkuu wa shirika hilo nchini Kenya Abbas Gulet ameambia BBC kuwa maeneo yaliyoahiriwa zaidi ni pamoja na Nairobi na maeneo yaliyo pembezoni, na garissa ambapo watu kadhaa wamefukiwa na maporomoko ya ardhi au kuzingirwa na maji.

Chanzo,BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...