Thursday, April 25, 2013

WATU 147 WAUWAWA KATIKA MKASA BANGLADESH

Maafisa nchini Bangladesh wamesema idadi ya waliofariki katika mkasa wa jengo kuporomoka imefikia 147 huku maafisa wa uokozi wakifanya kazi usiku kucha kutafuta watu waliokwama katika vifusi vya jengo hilo.Jengo hilo la orofa nane liliporomoka hapo jana asubuhi viungani mwa mji mkuu Dhaka katika eneo la Savar na inahofiwa mamia ya watu bado wamekwama chini ya vifusi vya jengo hilo lililokuwa na viwanda vya nguo.
Mashirika ya habari nchini humo yanaarifu kuwa watu waliripoti kuweko kwa nyufa kubwa katika jengo hilo siku moja kabla ya mkasa huo lakini wasimamizi wa jengo hilo inadaiwa hawakuchukua hatua zozote.Mkuu wa polisi katika eneo hilo Mohammed Asaduzzaman amesema polisi na baraza la mji huo wamewasilisha kesi tofauti dhidi ya mwenye jengo hilo kwa kutozingatia usalama.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI YA UJERUMANI

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...