Friday, April 26, 2013

Breaking news:GODBLESS LEMA AMEKAMATWA NA POLISI NA KUWEKWA NDANI.

 Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka Arusha ni kuwa Mbunge wa Arusha Mjini amekamatwa na kuwekwa ndani kituo cha kati Arusha. Kukamatwa kwake ni baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwake na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku  wa manane, lakini baadae Mh. Lema alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.
Kukamatwa  kwake  kulikuja  baada  ya polisi  kuvunja mlango na kuingia ndani  na  kuendesha  msako  wa  nguvu  humo  ndani .Vitu  kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police.
 
Hata hivyo, wananchi wengi walijitokeza wakati mbunge wao anakamatwa ambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani mchana wa leo.

Habari zaidi zitawajia kadiri tutakavyokuwa tunazipata.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...