Thursday, April 25, 2013

RAIS UHURU KENYATTA AZIDI KUTANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameendelea kulitangaza baraza lake la mawaziri. Katika uteuzi wa leo, Balozi Raychelle Omamo, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, huku Phylis Kandie akiteuliwa kuwa waziri wa uhusiano wa Afrika Mashariki na Utalii. Wengine walioteuliwa ni Charity Ngilu, ambaye atakuwa waziri mpya wa nyumba na makaazi, pamoja na Najib Balala, atakayekuwa waziri wa madini.Jumanne iliyopita, Rais Kenyatta, aliwateuwa mawaziri wanne, akiwemo Amina Mohamed, ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na Henry Rotich, aliteuliwa kuwa waziri mpya wa Fedha. Wiki iliyopita Rais Kenyatta alielezea muundo wa baraza lake utakavyokuwa, kwa kulipunguza baraza hilo kutoka mawaziri 44 hadi kufikia 18.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI YA UJERUMANI

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...