Thursday, April 18, 2013

REAL MADRID KLABU TAJIRI DUNIANI, YA PILI MAN UNITED

 Manchester United wameondolewa kwenye nafasi ya kwanza ya klabu yenye utajiri na thamani kubwa inayotolewa na jarida la Forbes.

United wamekuwa wakishika nafasi ya kwanza kila mwaka tangu Forbes walipoanza kutoa list ya vilabu vye thamani kubwa zaidi duniani mwaka 2004, lakini mwaka huu wameondolewa kileleni na Real Madrid - klabu ambayo iliitoa kwenye michuano ya champions league hive karibuni.

Barcelona wanashika nafasi ya tatu nyuma ya United, Arsenal wapo nafasi ya nne na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich wakikamilisha nafasi ya tano.

Real Madrid wanatajwa kuwa na thamani ya £2.15billion - na kwa namba hizo klabu hiyo ya Spain inakuwa ndio klabu ya michezo yenye thamani kubwa zaidi duniani - huku Manchester United wakiwa na thamani ya  £2.07billion.

Kwa upande wa wachezaji wa soka, David Beckham bado anaongoza kwa utajiri akiwa ameingiza kiasi cha kati ya £33m - £29m ambazo zimetokana zaidi na mikataba ya kibiashara ya matangazo.

Staa wa Real Madrid Ronaldo ameingiza kiasi cha (£28.8m) akishika nafasi ya pili, wakati mwanasoka bora wa dunia Lionel Mess akishika nafasi ya 3 kwa kuingiza jumla ya £26m mwaka jana kwa kupitia mshahara na mikataba ya kibiashara.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...