Pamoja na jana kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu
wa 2012/2013, kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na
mazoezi ya viungo na kujenga misuli (GYM) katika kituo cha mazoezi
kilichopo jengo la Quality Cetntre kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal
Union siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo jana
imetangazwa rasmi kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013
baada ya timu za Coastal Union na Azam FC kutoka sare ya bao 1-1,
imeendelea kujifua kuhakikisha inamalizia mzunguko wa pili wa VPL kwa
ushindi kama ilivyofanya tangu kuanza duru la pili.
Azam FC
iliyokua na ndoto za kuweza kufikia pointi 56 za Yanga, ilikua ikiombea
yenyewe kushinda michezo yake yote mitatu huku iikiombea Yanga kupoteza
michezo yake miwili iliyosalia hali ambayo ilikwenda kinyume hapo jana
kwa wauza mikate kupata sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union na kuifanya
Yanga itangazwe mabingwa wapya wa VPL kwa kuwa na ponti 56 ponti 8 mbele
ya Azam yenye pointi 48.
Huu
unakua ni Ubingwa wa 24 kwa Yanga tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu
Tanzania bara rekodi ambayo hakuna timu yoyote inayokaribia kufuatia
watani wa jadi Simba SC kuwa wametwaa ubingwa huo mara 18 tu.
Rekodi ya Ubingwa wa Yanga :1968,
1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991,
1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007-2008, 2008-2009,
2010-2011, 2012-2013
Baada ya kufanya mazoezi katika
uwanja wa shule ya sekondari Loyola kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku
ya jumatano, jana wachezaji waliingia kambini katika hosteli za klabu
zilizopo makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo wa
jumatano.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amekiongoza
kikosi cha wachezaji 26 kufanya mazoezi ya gym leo katika kituo cha
Quality Centre ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi
ya timu ya Coastal Union siku ya mei mosi jumatano katika uwanja wa
Taifa jijin Dar es salaam.
Yanga
imebakisha michezo miwili (Costal Union 01.05.2013) na (Simba SC
18.05.2013) kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodaom huku ikiwa tayari
imeshatwaa Ubingwa mapema kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom.
Uongozi
wa klabu ya Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya
Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya jumatano (mei mosi) katika dimba la
uwanja wa Taifa ili kuja kuwashangilia vijana wakiendeleza furaha ya
kutwaa Ubingwa wa VPL msimu huu.
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD, BACKWARD NEVER (EFBN)
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa Timu ya Yanga.
No comments:
Post a Comment