Kim Poulsen kocha mkuu wa Taifa Stars. |
Hii ni taarifa iliyotolewa na TFF kuwa Taifa Stars imealikwa kushiriki mashindano ya COSAFA na taarifa yenyewe ni hii hapa:-
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashiriki michuano ya Baraza la
Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika Julai
mwaka huu nchini Zambia.
Taifa
Stars inashiriki michuano hiyo ya timu za Taifa za nchi wanachama wa
COSAFA ikiwa timu mwalikwa. Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini,
Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius,
Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Michuano
hiyo itafanyika kuanzia Julai 6 hadi 21 mwaka huu katika miji ya
Lusaka, Ndola na Kabwe. Ratiba ya makundi ya michuano hiyo itapangwa Mei
3 mwaka huu jijini Lusaka.
Mara
ya mwisho michuano hiyo ilifanyika miaka mitatu iliyopita. Hii itakuwa
mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya kucheza ya
kwanza iliyofanyika mwaka 1996 nchini Zimbabwe.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajia kuingia
kambini mwishoni mwa mwezi ujao kujiandaa kwa mechi ya Kombe la Dunia
dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Juni
16 mwaka huu Taifa Stars itacheza na Ivory Coast jijini Dar es Salaam
katika mechi nyingine ya mchujo ya Kombe la Dunia wakati Juni mwishoni
na Julai mwanzoni itacheza mechi ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa
Ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.
Wakati
huo huo, waandishi wa habari wanaotaka kuripoti michuano hiyo
wanatakiwa kuwasilisha majina yao TFF kabla ya Aprili 27 mwaka huu ili
maombi yao yatumwe COSAFA kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho
(Accreditation).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment