Baraza la wafanyakazi MORUWASA lilifanya ziara katika hifadhi ya taifa ya Mikumi baada ya kumaliza kikao chake cha siku mbili katika Hoteli ya Chuo Cha VETA MIkumi.Hii ni rasili mali na hazina kwa Taifa letu,wote tushirikane kulinda na kuhifadhi.
Hapa ni bwawa kati ya mabwawa 3 yaliyochimbwa mbuni mikumi.Wanyama wanaopatikana ni Mamba,Kiboko na ndege maji |
Eneo la kuingilia mbugani Mikumi |
Pundamilia ambao kitu pekee kwao nikwamba wanasimama kila mmoja akiwa ameelekea upande wake kwa ajili ya usalama |
Hawa ni Tembo ambao wanapatikana kwa wingi mbugani Mikumi |
Hawa ni nyumbu ambao nao wanapatikana kwa wingi Mikumi. |
Hawa ni Twiga ambao kitu pekee kwao ni kuwa wakiwa wanatembea miguu ya upande mmoja inaenda pamoja tofauti na wanyama wengine ambao wanapishanisha miguu. |
Huyu ni kiboko aliyemo kwenye mabwawa yaliyochimbwa. |
Hawa ni nyati ambao wanasemekana kuwa wanya wakorofi hasa wakimuona mwanadamu. |
Mikumi kuna hata uwanja wa ndege,unaweza kutua moja kwa moja na ndege. |
Watu husema twiga huwa halali ukweli nikwamba analala kama anavyoonekana lakini hawezi kuinamisha kichwa,analala hivo hivo |
Hawa ni swala ambao wanapatikana kwa wingi Mikumi.Kitu cha pekee kwao ni kwamba dume moja unakuta linamiliki kundi kubwa la majike hata kuzidi idadi ya 100. |
No comments:
Post a Comment