Wafanyabiashara hao wakiwemo wanaomiliki maduka yanayolizunguka soko hilo, waliliambia gazeti hili kwamba takataka hizo zinatupwa nje ya soko.
Hata hivyo walalamikaji hao hawakutaka majina yao yatajwe lakini walisema takataka hizo zimerundikwa kwa muda mrefu bila ya kuzolewa na mamlaka zinazohusika.
Wafanyabiashara hao walisema katika kipindi hiki
ambacho mvua zimekuwa zikinyesha mfululizo mkoani humo, wamekuwa
wakizishuhudia taka hizo zikioza na hatimaye kutoa harufu mbaya.
Mkuu wa soko hilo, John Lugiza alikiri kuhusu kuwapo kwa taka hizo na kwamba ni kero hata kwa uongozi wa soko hilo.
Alisema kutokuzolewa kwa takataka hizo kunasababishwa na gari kushindwa kuingia ndani ya soko na kwamba dampo la Muriet nalo limejaa maji.
Habari hii kwa hisani ya Mwananchi.
No comments:
Post a Comment