Shirika la habari la taifa la Uchina linasema kuwa
watu 150 wamekufa katika tetemeko kubwa la ardhi ambalo limeporomosha
majengo na bara-bara katika jimbo la Sichuan, kusini-magharibi mwa nchi.
Wanajeshi kama 6000 wamepelekwa
kwenda kusaidia katika uokozi zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji
mkuu wa jimbo la Sichuan.
Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika.
Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo.
Tetemeko lilotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu 90,000.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment