Dr.Slaa akihutubia umati mkubwa katika mkutano jijini Mbeya. |
Katika kuendelea na ziara yao katika mikoa mbali mbali wabunge wa CHADEMA waliosimamishwa bungeni,jana wameendelea na ziara yao na kufanya mkutano mkubwa ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu mjini Mbeya.
Katika mkutano huo CHADEMA walimtahadharisha Rais kutokipigia debe Chama cha Mapinduzi.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi(Sugu) akihutubia mjini Mbeya. |
Mbunge wa
Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete
asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha
Mapinduzi(CCM)
bali afanye kazi za kiserikali.
Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya,Sugu alisema kuwa kitendo
hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.
“Wakazi wa
Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa
ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo
kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.
Mkutano huo
uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe, ulihudhuriwa pia na Katibu
Mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa, Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter
Msigwa (Iringa mjini), Ezekiel Wenje(Mwanza mjini) na Highness Kiwia wa
Jimbo la Ilemela. Sugu pia alitoa miezi mitatu kwa Halmashauri ya Jiji
la Mbeya kuhakikisha Soko Jipya la Mwanjelwa linakamilika ifikapo Julai
mwaka huu.
Alitishia iwapo kufikia muda huo halijakamilika yeye na wananchi wenzake watavamia soko hilo na kufanya kazi za ujenzi wenyewe.
Alitishia iwapo kufikia muda huo halijakamilika yeye na wananchi wenzake watavamia soko hilo na kufanya kazi za ujenzi wenyewe.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Peter Msigwa
alisema kuwa wamejipanga kufanya maamuzi magumu kama Spika wa Bunge,
Anne Makinda
ataendelea kuwapendelea wabunge wa CCM.
ataendelea kuwapendelea wabunge wa CCM.
Dk Willbroad Slaa alisema sababu ya wabunge wa Chadema kufukuzwa bungeni ni
kutokana na kutekeleza majukumu waliyotumwa na wananchi.
Aliwataka
Wananchi kuendelea kuwaunga mkono na watambue kuwa CCM na Serikali yake
inafanya kazi ya kutetea ubovu wa Serikali na kuwafanya Watanzania kuwa
katika hali ya
umasikini huku walionacho wakizidi kuneemeka.
umasikini huku walionacho wakizidi kuneemeka.
Wabunge wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliosimamishwa bungeni wiki
iliyopita wameamua kwenda kuwashitaki Spika Anna Makinda na Naibu wake
Job Ndugai kwa wananchi kwa njia ya kuitisha mikutano ya mihadhara.
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa CHADEMA.
No comments:
Post a Comment