Wednesday, April 17, 2013

MH. GODBLESS LEMA BAADA YA KUONGEA KWA MARA YA KWANZA BUNGENI, AZUA MVUTANO MKALI NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.

Mh.Godbless Lema.
Kwa mara ya kwanza akiongea Bungeni lililokuwa linaongzwa na Naibu spika Mh.Jobu Ndugai,baada ya kuwa likizo ya muda mrefu kutokana na kuvuliwa ubunge wake, mchango wake bungeni umezua tafrani jambo lililozua mvutano mkali kati ya Lema,Waziri Lukuvi, Tundu Lisu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akitoa mchango wake, Mh.lema amesema kuwa Kiongozi mkuu wa CCM ambaye ni Rais Kikwete na viongozi wenzake wa CCM ni vinara wa kuchochea UDINI na UKABIRA hapa nchini.

Akithibitisha hilo, alisema kuwa CCM wanasema kwa wananchi kuwa CHADEMA ni chama cha udini na ni cha Wakristu na pili kuwa CHADEMA ni chama cha ukabira jambo mambo ambayo yanapelekea mpaka kwenye mgogoro wa nani achinje na nani asichinje.
Pia alisema anahofia usalama wa Kucha zake, meno yake na kope zake baada ya usalama wa taifa kutesa watu an kuwatoa kope,kucha na meno watu mbali mbali.

Baada ya kusema hayo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Bunge, Wiliam Lukuvi,aliomba mwongozo kuhusu Mh.Lema Kumdhihaki Rais Kikwete na kwa kumtaja kwa jina kuwa kanuni ya 64 inakataza.

Akijibu hoja hiyo, Mh.Lema alisema kuwa hajamdhihaki Rais bali ametumia maneno makali ambayo ni ya kukosoa.

Baada ya malumbano hayo, ndipo mwanasheria mkuu wa serikali aliposimama na kumtaka mh.Lema aidha afute kauli yake au Mh.Naibu spika atoe mwongozo.

Baada ya maneno hayo kutoka kwa Mwanasheria mkuu wa serikali, ndipo mnadhimu mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani Mh.Tundu Lissu aliposimama na kutoa ufafanuzi wa jambo hilo kuwa,kutokana na kanuni ya 64.1(d) inakataza kutumia jina la Rais kwa dhihaka lakini sio kukataza kumshauri Rais,na neno dhihaka ni kumkejeri mtu mfano kusema msanii, labda kama tunabadilisha badala ya dhihaka iwe vinginevo.Mh.Lema hajamdhihaki Rais bali ametumia maneno makali kwa Rais.
Ndipo Naibu spika aliposema kuwa watanzania wanaliangalia bunge,kama kila mmoja atasema kama bunge lilivyokubaliana kila kitu kitaenda sawa,hivyo akamuomba mchangiaji ajikite kwenye hoja.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...