Sunday, April 21, 2013

WARAKA WA NDUGU GOLDEN CHARLES MARCUS KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA



GOLDEN CHARLES MARCUS
WARAKA WANGU KWA SERIKALI, TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NA WANANCHI KWA UJUMLA
(Kwenye Mitandao ya Kijamii:- Gmail, Yahoo, Facebook, YouTube, Amazon, Twitter na AOL)
Mwanzo Kabisa, kabla hata ya kuanza Mchakato wa Kupata Katiba Mpya, Tume ya Mabadiko ya Katiba ilitafuta na kupata na kutumia Kaulimbiu isemayo TOA MAONI, TUPATE KATIBA MPYA, na Dira yake ilikuwa KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA KATIBA MPYA huku Dhamira yake ikiwa ni KURATIBU, KUKUSANYA NA KUTHAMINI MAONI YA WANANCHI ILI KUPATA KATIBA MPYA.

Tume hiyo ya Katiba ikaanza Kazi mara moja kwa Ukusanyaji wa Maoni ya makundi mbalimbali mnamo tarehe 7 – 25 January, 2013, baada ya hapo ilichambua Maoni ya Wananchi mnamo 3 Februari – 4 Machi, 2013, Mnamo tarehe 4 Aprili ikaanza Uandishi wa Rasimu ya Katiba ambayoitashia 2 Mei, 2013.
Lakini licha ya Mipango hiyo mizuri ya Tume, kuna baadhi ya vitu vinafanyika / vimefanyika bila mtazamo mkubwa na wakina na wandani zaidi kwa sababu Wananchi ndiyo watoa Maoni na ndiyo wapendekezaji wakubwa katika hatua hizo za Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Tume ilianzisha mchakato wa kuandaa mabaraza bila kufikilia kwa mapana zaidi kuwa, kilichotakiwa kufanyika ni:-
Kutoa tangazo kwa Wananchi ili watume maombi – hili lilifanyika Vizuri
WDC (Baraza la Maendeleo la Kata la Wenyeviti wa Mitaa na Madiwani husika) walitakiwa wachambue maoni na kupitisha watu wenye sifa husika kwenda kuhakikiwa na Wananchi, kisha Wananchi ndiyo watoe maamuzi ya nani atakayekuwa muwakilishi wao au Uteuzi wa moja kwa moja kutoka kwa Wananchi, sasa mambo yakawa kinyumenyume ikaanza kwa Wananchi nao kwakuwa hawajui kinachoendelea Wakateuwa na kuwaamini Watu watakao wawakilisha, baada ya Wananchi kuchagua watu watakao wawakilisha, Baraza hilo la WDC likatengua maamuzi ya Wananchi na kufanya Uchaguzi upya bila Wananchi kujua (Mchuujo), huku Wananchi wakiamini wamemaliza kupeleka Wawakilishi wao!! kwa namna hii unafikili DIRA na DHAMIRA ya TUME YA KATIBA itafikia malengo?
Mbali na hayo, kazi hii ya Uchaguzi au Muundo wa Mabaraza ulikuwa ni wa KITAIFA badala yake umefanyika kwa UDINI, UCHAMA, RUSHWA na UDANGANYIFU MKUBWA, kwa jinsi hiyo imepelekea Wananchi wengi kupoteza Imani na Tume, kwa mfano Kata ninayotoka mimi GOLDEN CHARLES MARCUS Kata ya Kitaji Musoma Mjini hayo yalijionesha wazi wazi na nilijaribu kuomba Muongozo wa Tume kama yanayofanyika ni sahihi kwa kutuma sms kwenye Namba 0715 081508, 0767 081508, 0787 081508, 0774 081508 (namba hizi ni za Tume) bila majibu yoyote.
Katika Kata yangu kuna Mitaa minne yaani Kitaji ‘A’, ‘B’, ‘C’ na ‘D’ pamoja na Madiwani watatu, wakuchaguliwa mmoja, viti maalum wawili, 02/04/2013 ulifanyika Uchaguzi wa Wawakilishi wa Mabaraza katika Ngazi ya Mtaa, kwenye kundi langu nililoomba la kuwakilish Vijana nilichaguliwa na Wananchi kutoka Mtaa wa Kitaji ‘C’ kwa Kura 120 huku aliyenifuatia alikuwa na kura 97, baada ya Uchaguzi huo wa Tarehe 02/04/2013, tulikutana tena kwenye Mchuujo wa Ngazi ya Kata (WDC) 08/04/2013 lakini kulikuwa na mama mmoja ambaye ni Mwl. Wa shule ya Msingi Azimio na anaishi hapo hapo shule ina maana ni 

Mtumishi wa Serikali kadhalika Mme wake ni Trafki (Polisi wa Usalama Barabarani) na si Mkazi wa kudumu wa Kata husika kama Tangazo la Maombi lilivyoahinisha, kwa jinsi ninavyojua kuwa Mtumishi wa Serikali haruhusiwi kuwania nafasi kama hiyo nakama angekuwa mkazi wa kawaida, kwa sehemu anayoishi ilimpasa mama huyu kugombea Kitaji ‘C’ sababu shule anayoishi hiko Kitaji ‘C’, lakini alitumia pesa kwa M/kiti wa Kitaji ‘C’ na Kitaji ‘B’ akafanyiwa mpango na kapita kwa mabavu na ujanja ujanja mwingi na udanganyifu Mkubwa akawa ameshindia Kitaji ‘B’ ambayo kitaratibu shule anayoishi haiku huko ina maana si Mkazi wa ‘B’.
Wakati tunasubiri Kikao hicho cha kutengua maamuzi ya Wananchi cha 08/04/2013 mama huyo na Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata hii kilitangaza Uchama sana na hata kufanya Vikao vya Usiku na Mchana kupanga safu yao waliyoitaka, huku Wagombea kutoka Chama hicho wakifanya Kampeni chafu za Rushwa na Uchama Usiku na Mchana mpaka nikajuta kugombea, nanikajiuliza kama hali ilikuwa hivyo kwanini kazi hii wasingewapa watu wa CCM au Watu ambao wamewaanda kuliko kutangazia UMMA halafu wao wanapanga Orodha ya Majina ya Watu ambao wanawataka na kweli inakuwa hivyo huku Wananchi wakiwa wameduwaa kwa Matokeo ya Mchuujo.

Kwa Upande wangu nilishangaa sana na kwa hatua hiyo Wananchi walio wengi itakuwa ngumu kwao kuamini Kaulimbiu, Dira na Dhamira ya Tume, Hivyo kwa Waraka huu Tume iangalie chakufanya mapema, kama kubatilisha Uchaguzi huu, ama vinginevyo kwa kadri ya Maamuzi ya Wananchi wengi, waliopiga kura na kubatilishwa na Wachache (WDC) kwa manufaa yao, itakuwa Ngumu kwa Wananchi, hii imeonekana wazi kuwa, ni namna gani Uongozi mdogo wa Chini unavyochonganisha Wananchi na Viongozi wa Juu wa Taifa kama Mchezo huu utakuwa hahukusukwa toka juu, kwa Uchaguzi huu wa wawakilishi wa Mabaraza katika Kata yangu ya Kitaji – Musoma, hauko mbali na Matokeo ya Kidato cha Nne, yaani waliofanya Mahojiano yaani kujieleza mbele ya Baraza (WDC)  hawakuchaguliwa (wamefeli) lakini ambao hawakuwepo na walikuwa wameshatengeza Mazingira Mazuri (Kampeni + Rushwa + Uchama) na hawakujieleza, wameshinda!!!!   
 hii nini au Hili ni Taifa gani tunaloliandaa?.
MWISHO:
Wananchi ndiyo watumiaji wa Katiba na ndiyo wenye maamuzi makubwa, Waheshimiwe na kusikilizwa katika maamuzi yao.
GOLDEN CHARLES MARCUS
Mteule wa Wananchi – Kitaji ‘C’
0767 328202 / 0784 328202 / 0777 328202 / 0658 284625
(Kijana Mwenye Uchungu na Taifa

CHANZO,Mtandao wa kijamii wa CHADEMA

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...