Monday, April 22, 2013

MAPIGANO NIGERIA 185 WAFARIKI DUNIA


Wapiganaji wa Boko Haramu
Mapigano ya wapiganaji wa kiislamu na vikosi vya usalama nchini Nigeria yameripotiwa kutokea tangu usiku wa Ijumaa na kuendelea kwa muda mrefu ambapo jumla ya watu 185 wanaripotiwa kufariki dunia katika mapigano hayo yaliyotokea Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole,inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea. Brigedia Jenarali Austin Edokpaye amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makazi ya watu ambapo walijua vikosi vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na vifo vya raia wengi tangu kuibuka kwa vikundi vya wapiganaji wa kiislamu mwaka 2010 ambapo vingi vimejikita Kaskazini mwa nchi hiyo.

CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...