Pia, alitoa onyo kwa makandarasi wababaishaji
ambapo amesema hatavumilia kuona Tanzania inafanywa kichaka cha watu
wanaokuja kuchota fedha za bure na kuondoka pasipo kutimiza majukumu
yao, ambayo yanakuwa yameainishwa kwenye mikataba wanayoingia na
Serikali.
Waziri Mwakyembe alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akishuhudia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ikisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza katika halfa hiyo, Mwakyembe alisema
ujenzi wa jengo hilo ni faraja kubwa kwa Serikali ya Tanzania, kwani
litasaidia kuongeza ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa Watanzania.
Alisema licha ya Serikali kupongeza jitihada hizo za TAA asingependa kuona ujenzi wa jengo hilo ukifanywa chini ya kiwango kwani huu ni wakati wa kuhakikisha kila kitu kinachofanyika nchini kinafanywa kwa viwango vya hali ya juu. Mwakyembe aliiagiza TAA kusimamia mradi huo uweze kumalizika kwa muda uliopangwa na kwamba idhibiti ubadhirifu wowote wa mali zitakazotumika katika mradi huo.

Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo Kaimu
Mkurugenzi wa TAA, Suleiman Suleiman alisema ujenzi huo utafanyika kwa
awamu mbili na kwamba hadi kukamilika kwa jengo hilo litakuwa na uwezo
wa kuchukua abiria milioni sita. “Jengo la abiria lina uwezo wa kuchukua
abiria zaidi ya milioni moja lakini tunapata faraja kwamba pindi ujenzi
huu utakapo kamilika uwanja wa JNIA utakuwa na uwezo mkubwa wa kuchukua
abiria wengi na kwamba ni faida kwa uchumi wa nchi yetu,”alisema
Suleiman.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bam
International Martin Bellamy alisema wamepata faraja kushinda zabuni
hiyo na kwamba wao kama wenyeji hapa nchini watahakikisha wanafanikisha
mradi huo. Jengo hilo linajengwa na Kampuni ya Bam Inenationali ya
Uholanzi kwa gharama ya Sh275 bilioni ambapo hadi kukamilika litakuwa na
uwezo wa kuchukua abiria milioni sita.
Chanzo, Mwananchi.
Chanzo, Mwananchi.
No comments:
Post a Comment