Saturday, April 13, 2013

VITA KALI BUNGENI TUNDU LISU vs MWIGULU MCHEMBA


Mh.Mwigulu mchemba.
Mh.Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) aliishambulia hotuba ya Mbowe akieleza kuwa hakuna haja ya kuhangaika na suala la ugaidi kwa kuwa Chadema ndiyo wanahusika nalo kwa kupanga kumdhuru mwandishi wa habari.

 “Watu wanapanga ugaidi halafu wanaachiwa tu, nashukuru Mbowe hayuko hapa nadhani atakuwa amekamatwa pamoja na katibu wake kwa kuwa wao ndio wamekuwa wakiwasiliana na aliyekuwa amepanga ugaidi,” alisema Nchemba.

Naye Tundu Lissu.
Mh.Tundu Lissu.
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), akichangia hoja hiyo ya ugaidi, “...Kuna mheshimiwa humu ndani aliwasiliana na gaidi,” alisema Lissu kabla ya Anne Abbdalah kumtaka athibitishe na Lissu alisema: “Ushahidi upo kama Anna Abadallah anataka, kwani malipo yalifanywa na magaidi waliopo humu ndani..”

Pia Lissu amekuja juu na kusema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anatakiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa kuwa ameshindwa kumwajibisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Amesema kitendo cha Waziri Mkuu kushindwa kumwajibisha Dk. Kawambwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, hakiwezi kuvumiliwa na hivyo wabunge wanatakiwa kumwajibisha Waziri Mkuu.

Lissu aliyasema hayo bungeni jana, alipokuwa akichangia bajeti ta Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Pamoja na kutaka hatua hiyo ichukuliwe, Lissu alisema tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne umeshuka ikilinganishwa na hali ilivyokuwa enzi za Rais Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa Lissu, mwaka jana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilitoa ripoti ya takwimu za ubora wa elimu nchini kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka juzi ikionyesha kushuka kwa ufaulu nchini.

Alisema ripoti hiyo, inaonyesha katika kipindi cha miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Serikali ya awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ufaulu wa wanafunzi ulipanda.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...