Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Waziri mkuu wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa
Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya
nchi mbili hizo.
Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa
Afrika Kusini kuuwawa mwezi Machi wakati wapiganaji walipoiteka serikali
ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment