Wednesday, April 24, 2013

ZITTO KABWE NA BAJETI YA WIZARA YA MAJI.

 Ktika akaunti yake ya mtandao wa kijamii,Mh.Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kasikazini, kaelezea kwa ufupi mchanganuo na vipaumbele vya Wizara ya maji katika bajeti ya 2013/2014 na kuandika yafuatayo:-  
"Bungeni Leo na kesho Ni bajeti ya Wizara ya maji. Waziri ametaja mipango mingi sana kwenye hotuba yake. Hata hivyo ukiangalia pesa za bajeti unaona mipango mingi Ni porojo tu. Kwa mfano, kupitia mpango wa "tekeleza sasa Kwa matokeo makubwa" Serikali imepanga kufikisha maji Kwa wananchi 15.4m ifikapo mwaka 2016. Mpango huo utagharimu jumla ya tshs 1.5trn. Hata hivyo ukiangalia Bajeti nzima ya Wizara Ni tshs 398bn tu ambapo tshs 379bn Ni za maendeleo (hii Ni kudos maana Fedha za miradi Ni nyingi kuliko za matumizi ya kawaida). Hata hivyo tshs 241bn Ni kutoka Kwa wafadhili. Bajeti yote ya Wizara ya Maji Ni 2.2% ya Bajeti nzima ya serikali inayofikia takribani ths 18trn. Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Maji ndio tatizo kubwa zaidi linalokabili Watanzania. Wakati wa Bajeti ya Waziri Mkuu, wabunge wengi walichangia kuhusu matatizo ya maji katika maeneo yao kuliko suala lingine lolote lile. Ninaamini wabunge watajadili hotuba ya Waziri wa Maji Kwa kuzingatia unyeti wa suala hili ili kuwaondolea adha wananchi wa vijijini na hasa wanawake wanaohangaika kutafuta maji umbali mrefu sana. Maji Ni Uhai......"

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...