Mohamed Dewji. |
Katika kuhakikisha kuwa Taifa stars inafuzu na kushiri fainali za kombe la Dunia huko Brazil, Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo imeteua kamati ya Ushindi kama ifuatavyo:-
"Kama
mnavyofahamu, hivi sasa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa Wanaume
(Taifa Stars) ipo kwenye michuano ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe
la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Katika
Afrika, Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C kati ya makundi 10.
Kundi C linajumuisha timu za Ivory Coast, Morocco, Gambia na Tanzania.
Kwa
sasa katika kundi C, Taifa Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na alama
sita (6), nyuma ya Ivory Coast yenye alama saba (7), Morocco ina alama
mbili (2) na Gambia ina alama moja(1).
Kwa
mara nyingine Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapenda
kuwapongeza Taifa Stars, kwa kazi nzuri ambayo wameishaifanya ikiwemo
ushindi wa Bao Tatu kwa Moja dhidi yaMorocco. Watanzania wote na Wadau
wa Soka nchini wamefurahishwasanana mafanikio yaliyofikiwa na Taifa
Stars na yenye kutupa matumaini katika kuitayarisha Taifa Stars kufuzu
kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014 nchiniBrazil.
Kwa
hali ilivyo hivi sasa, Taifa Stars ipo katika nafasi nzuri ya kufuzu.
Ili Tanzania tuweze kufuzu, Taifa Stars inatakiwa ishinde mechi zote
tatu (3) na kuongoza kundi C na baadae iingie katika Timu kumi (10) bora
na kisha zipatikane Timu tano (5) kutoka Afrika ambazo zitakuwa
zimefuzu kwenda Brazil katika Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014.
Tunaamini hili linawezekana.
Sasa
kwa kuzingatia uzito wa jukumu lililo mbele yetu na kwa Taifa Stars kwa
ujumla; Serikali imeunda Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars.
Jukumu
la msingi la Kamati tunayoiunda ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa
na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha
kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati ya
Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa
wafuatao:-
1. Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
2. Bi. Teddy Mapunda - Montage
3. Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
4. Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
5. Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
6. Bw. George Kavishe - TBL
7. Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
8. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
9. Bw. Joseph Kusaga - Clouds
10. Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
11. Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge
Kamati
hii iliyoteuliwa leo, naomba ianze kazi mara moja. Hadidu za rejea
zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati
itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa.
Serikali
inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii
inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote
zilizombele yetu.
Aidha
nichukue fursa hii kutoa wito kwa Watanzania wote, kuiunga mkono Taifa
Stars na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars kwa hali namalikatika
kuhakikisha timu yetu inafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu naomba
niwasilishe salaam zao za kuwapongeza Vijana wetu wa Taifa Stars,
pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Kim Poulsen. Kwa
pamoja wanaomba Taifa Stars iendelee kujipanga kwa mechi zijazo.
Nawahakikishia kuwa Serikali, Watanzania na wadau wa Soka nchini wapo
nyuma yao.
Mungu Ibariki Taifa Stars.
Mungu Ibariki Tanzania.
Dkt. Fenella Mukangara (Mb)
WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
16 Aprili, 2013"
No comments:
Post a Comment