Kutokana na habari aliyoitoa Afisa Habari wa TFF, ni kwamba mechi zilizokuwa zioneshwe hii leo na kesho hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.Taarifa kamili hii hapa:-
"Mechi
tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa
zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport
cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.
Kwa
mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport
Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha
mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya
kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya,
Tanzania na Uganda.
Mechi
hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na
Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga
itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.
Tatizo
hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo
hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya
televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.
Tshunungwa
amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo
hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga
mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Pia
TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa
waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya
Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)"
No comments:
Post a Comment