Antony Lutta - Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora |
Akiongelea tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Lutta, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.
Lutta alisema mtuhumiwa alimfumania mke wake Veronica Maganga (20) akiwa chumbani kwake na mwanamume mwingine .
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwanamume huyo alifanikiwa kukimbia.
Alisema hasira za mtuhumiwa katika tukio hilo ziliishia kwa kumtakata mke kwa panga hadi alipokufa.
Kamanda Lutta aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi mwao na badala yake, waviachie vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.
“Watu wamekuwa na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwahukumu watuhumiwa, huo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi na tunawasihi waache,” alisema kamanda huyo.
Alisema mtuhumiwa wa tukio hilo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Habari hii ni kwa hisani ya Mwananchi.
No comments:
Post a Comment