Polisi nchini Kenya wameelezea BBC kuwa watoto 2 wamekwama nyumbani
kwao baada ya kufukiwa na tope na maji yaliyosababisha maporomoko ya
ardhi.
Watoto
hao walikuwa wamelala katika kijiji cha Narok kilomita kadhaa kutoka
mji wa Nairobi, mvua kubwa iliponyesha na kusababisha maji kusomba
majumba kadhaa katika mtaa wao.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya
limeonya watu wanaoishi maeneo yanayotishiwa kukumbwa na mafuriko
wahamie sehemu za juu na milima.
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika sehemu nyingi nchini humo na inaaminiwa kuendelea kunyesha.
Katibu mkuu wa shirika hilo nchini Kenya Abbas
Gulet ameambia BBC kuwa maeneo yaliyoahiriwa zaidi ni pamoja na Nairobi
na maeneo yaliyo pembezoni, na garissa ambapo watu kadhaa wamefukiwa na
maporomoko ya ardhi au kuzingirwa na maji.
Chanzo,BBC
No comments:
Post a Comment