Bunge la Ufaransa limeidhinisha ndoa za watu wa jinsia moja na
kuruhusu wanandoa hao kupata watoto wa kupanga.Bunge hilo la
Ufaransa lenye wabunge wengi wa kisosholisti liliupigia kura mswada
huo kwa kura 331 dhidi ya 225 ili kuidhinisha kuwa sheria.Sheria
hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Juni
mwaka huu.Baada ya kura hiyo wakereketwa wanaounga mkono
ndoa za watu wa jinsia moja walisherehekea uamuzi huo wa bunge
na kusema wanastahili kuwa na uhuru wa kufanya maamuzi ya jinsi
ya kuendesha maisha yao na kuwa uamuzi huo wa bunge umewapa
uhuru huo.Hata hivyo kumekuwa na upinzani wa kupitishwa kwa
sheria hiyo mpya.Punde baada ya kuidhinishwa,wabunge kutoka
vyama vya mrengo wa kulia walitangaza kuwa wataupinga
kikatiba.Baraza litakuwa na mwezi mmoja kutoa uamuzi
kamili.Ufaransa ni nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia
moja duniani.
CHANZO:IDHAA YA KISWAHILI YA UJERUMANI.
No comments:
Post a Comment