ZITTO KABWE ASIGINA BAJETI YA WIZARA YA MAJI ILIYOONGEZEWA BIL.184.5
Baada ya bajeti ya Wizara ya maji kuongezewa kiasi cha Tsh.bilioni 184.5 kama ilivyokuwa imeshauriwa na kamati ya bunge hapo awali,bado mgawanyo wa kifedha kwenye bajeti hiyo umeonekana kutokuwa na usawa kulingana na mgawanyo wa watu kati ya mijini na vijijini.
Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh.Zitto Kabwe (CHADEMA) ametoa muhtasari wa mgawanyo wa kifedha katika bajeti hiyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kama ifuatavyo:-
"Maji
Bajeti yake ya 2013/14 licha ya nyongeza ya tshs 184.5 bilioni, bado
mgawanyo wa Bajeti ya Maji umeegemea sana mijini. Kabla ya nyongeza ya
bajeti, miradi ya mijini ilikuwa imepangiwa tshs 254bn wakati miradi ya
vijijini ilipangiwa tshs 75bn tu. Baada ya kelele za Wabunge, miradi ya
vijijini imepangiwa tshs 237bn wakati mijini imepanda mpaka tshs 266bn.
Watanzania 74% wanaishi vijijini, lakini mgawo mkubwa unakwenda mijini.
Lazima sasa tuweke uwiano wa mgawo wa rasilimali za kibajeti kulingana
na wapi wapo Watanzania wengi. Watu wa vijijini wanaminywa sana. Mwalimu
aliwahi kuonya kuwa "tusisahau maendeleo ya vijiji" tusiruhusu miji
kunyonya vijiji kimaendeleo."
No comments:
Post a Comment