Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana),
Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema
(Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chanzo cha kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba hakuweza
kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa
Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao
walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari kuongezwa.
Mapema Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter
Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa hotuba ya Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kupiga mkwara wa kuwashughulikia
wabunge watakaorusha matusi.
Serukamba
Serukamba alipewa nafasi ya kutoa taarifa wakati wabunge walipokuwa wakilumbana juu ya uhalali wa Msemaji wa Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi kuzungumzia bungeni masuala yaliyoko mahakamani na shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa.
Serukamba alipewa nafasi ya kutoa taarifa wakati wabunge walipokuwa wakilumbana juu ya uhalali wa Msemaji wa Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi kuzungumzia bungeni masuala yaliyoko mahakamani na shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa.
Wakati akijiandaa kusoma vifungu vya kukatiza
hotuba ya Profesa Kahigi, alitukana tusi zito la nguoni kwa lugha ya
kimombo ambalo kwa sababu za kimaadili hatukuweza kuliandika, kisha
akaendelea kuzungumza huku baadhi ya wabunge wakipigwa butwaa.
Hata hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai aliyekuwa
akiongoza shughuli za Bunge wakati huo, hakutoa karipio lolote huku
akimruhusu Serukamba kuendelea kwa muda kabla ya kumkatiza na kumruhusu
Mbunge wa Simanjiaro (CCM), Christopher Ole Sendeka kuzungumza.
Ubishi ulivyoanza
Muda mfupi kabla ya Profesa Kahigi kuanza kusoma hotuba yake, Serukamba alisimama na kuomba mwongozo wa Spika kupitia Kanuni ya 68(1) akitaka isisomwe kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa nne kwa kuwa unaingilia uhuru wa Mahakama... “Ni juzi tu Akoonay (Mustapha, Mbunge wa Mbulu - Chadema), alitukumbusha kwamba mambo hayo ni ‘prejudice’ kwa Mahakama kwa hiyo ukiruhusu hilo Naibu Spika itakuwa ni ajabu.”
Muda mfupi kabla ya Profesa Kahigi kuanza kusoma hotuba yake, Serukamba alisimama na kuomba mwongozo wa Spika kupitia Kanuni ya 68(1) akitaka isisomwe kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa nne kwa kuwa unaingilia uhuru wa Mahakama... “Ni juzi tu Akoonay (Mustapha, Mbunge wa Mbulu - Chadema), alitukumbusha kwamba mambo hayo ni ‘prejudice’ kwa Mahakama kwa hiyo ukiruhusu hilo Naibu Spika itakuwa ni ajabu.”
Kabla Naibu Spika hajatoa mwongozo wake, alimtaka
Profesa Kahigi kuzungumza kama anakubaliana na Serukamba, lakini Profesa
Kahigi alisema anaomba kuendelea kusoma hotuba yake kama ilivyo.
Baadaye Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika
aliomba kumpa taarifa Serukamba kwamba katika kurasa alizozitaja hakuna
jambo lolote lililopo mahakamani hivyo aangalie vizuri.
“Mheshimiwa Naibu Spika napenda kumpa taarifa mtoa
taarifa kwamba hakuna lolote lililopo mahakamani, ukurasa wa kwanza
unazungumzia Idara ya Usalama wa Taifa, haipo mahakamani, ukurasa wa
pili umemtaja Dk Stephen Ulimboka, halipo mahakamani hivyo hakuna lolote
lililopo mahakamani,” alisema.
Baada ya hapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kueleza kuwa
aliyoyasema Serukamba ni kwamba hotuba hiyo inafanya kesi iliyopo
mahakamani kuwa ya kisiasa akisema... “Kifungu cha 16 cha Sheria ya
Usalama wa Taifa hakiruhusu watumishi wa Usalama wa Taifa kutajwa humu
ndani wala kuchapishwa popote.”
Naibu Spika alisimama na kusema jambo hilo
limeshajitokeza ndani ya Bunge na Akoonay alishawakumbusha kuwa ni
kuingilia Mahakama.
“Jambo hili lilishaleta kasheshe humu ndani
na ruling (uamuzi) ya hili ilishatolewa na Spika, ‘ruling’ yangu ni
kwamba kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa nne, mambo ya Dk Ulimboka,
Usalama wa Taifa na Lwakatare.........,” aliishia hapo Ndugai na
kuwaruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Ole
Sendeka kuzungumza.
Mdee alisema ukurasa wa kwanza mpaka wa tatu wa
hotuba hiyo hakuna sehemu jina la Lwakatare lilipotajwa na kwamba
ukurasa wa nne uliotaja jina la Lwakatare hauzungumzii mwenendo wa
kesi... “Hoja anazoleta Lukuvi atusomee hiyo Sheria ya Usalama na
atuelezee na alinganishe na kilichopo hapa.”
Mdee aliungwa mkono na Lissu aliyesema kuwa sheria
anayozungumzia Lukuvi ipo lakini haikatazi kutajwa majina ya
wanausalama ndani ya Bunge... “Ninayo hiyo sheria hapa ya mwaka 1996,
haya maneno kwamba Sheria ya Usalama inakataza masuala ya Usalama wa
Taifa kutajwa ni uchochezi. Hicho kinachoelezwa kukataza ‘disclosure’
(kuwataja) ni huko nje na si humu ndani.”
Lissu alisema sheria hiyo inakataza kuchapishwa majina hayo nje ya Bunge na si vinginevyo.
Kairuki alipingana na Lissu akieleza kuwa
amepotosha kwa kuwa sheria hiyo ya Usalama wa Taifa hairuhusu kuwataja
watumishi wake bila kuomba ruhusa kwa waziri.
“Lissu anapotosha kwa kuwa hairuhusiwi mtu yeyote
kuchapisha jina la mtumishi wa Usalama wa Taifa bila kuomba ruhusa kwa
waziri,” alisema Kairuki.Ndipo Naibu Spika alipompa tena nafasi
Serukamba na alipoanza tu kuchangia kuliibuka maneno ya chinichini
ambayo yalionekana kumkera ndipo alipotoa neno hilo zito.
Baadaye Ndugai alisema kwa kuwa hilo suala ni la kikanuni, anaiagiza Kamati ya Kanuni ikutane ili tujadili suala hilo.
Katika hotuba hiyo ambayo awali, waandishi
walipata nakala yake, Profesa Kahigi alikuwa ameandika mambo mbalimbali
yanayohusu kutekwa na kuteswa kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari
Tanzania, Dk Steven Ulimboka na masuala mengine yanayohusiana na kesi ya
ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare.
Chanzo,Mwananchi.
Chanzo,Mwananchi.
No comments:
Post a Comment