Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, Boko Haram , limekataa pendekezo la kukubali msamaha.
Wiki jana Rais Goodluck Jonathan, aliuomba
mkutano wa maafisa wakuu wa usalama kutafakari swala la kuwapa msamaha
wapiganaji hao ili kuwashawishi kusitisha harakati zao.Tangazo na mtu anayeaminika kuwa kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau.
Katika miaka ya hivi karibuni, Boko Haram imekuwa ikiendesha kampeini ya ghasia na vurugu katika eneo la Kaskazini mwa nchi, na kuwaua takriban watu 2,000.
Kundi hilo linasema kuwa wapiganaji wake wanapigania kile wanachosema ni taifa la kiisilamu katika eneo la Kaskazini ambalo lina idadi kubwa ya waisilamu.
Bwana Shekau alisema kuwa kundi lake halijakosa hata kidogo, na kwa hivyo msamaha kwao sio jambo la kuzungumzia.
Aidha Shekau aliongeza kuwa ni jeshi la Nigeria ambalo linakiuka haki za waisilamu.
"nashangazwa kwa kuwa serikali ya Nigeria inazungumzia kuhusu msahama. Sisi tumefanya makosa gani? Ni sisi ambao tunapaswa kuwasamehe.'' alinukuliwa akisema Shekau
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria,Will Ross, anasema kuwa viongozi wa kisiasa na kidini Kaskazini mwa nchi, wamekuwa wakimtaka rais Jonathan kuwasamehe wapiganaji hao, wakisema kuwa hatua za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao hazisaidii kuleta amani.
Jopo la kutoa msahama liliundwa na serikali wiki jana na linajumuisha waakilishi wa jeshi.
Habari hii kwa hisani ya BBC
No comments:
Post a Comment