Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasifu
wabunge wa chama hicho waliosimamishwa huku akimshambulia Spika wa
Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kuwa wanaliendesha Bunge
kiharamia.
Akizungumza
jana katika uzinduzi wa M4C ya CCADEMA kwa Kanda ya Kati, Mbowe alisema Spika
Makinda amekuwa ni mwongo hata kuidanganya dunia kuwa uamuzi wao ni
sahihi jambo ambalo si kweli.
“Spika
Makinda ni mwongo, ameidanganya dunia na amekuwa akitumia maneno ya
uongo kuhalalisha uharamia uliofanywa na Naibu Spika wa Bunge kwa
kuwatoa ndani wabunge watano wa Chadema,”alisema na kuongeza:
“Uhuni kama
huu ndugu zangu haukubaliki, tutaendelea kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha tunatetea masilahi ya nchi hii na watu wake. Na hapa
natangaza mbele yenu kuwa wabunge walioondolewa ndani ya Bunge ni
mashujaa,” alisisitiza Mbowe.
Mbowe ambaye
ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, aliwaambia wanachama na
mashabiki wa Chadema kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu ndani
ya Bunge na kwamba wanatakiwa kuwa majasiri wakiwa bungeni.
Alisema
kwamba wakati wote wamekuwa wakishutumiwa kuwa wanafanya fujo ndani ya
Bunge, jambo alilosema siyo kweli bali wao wanasimamia Kanuni za Bunge
ambazo zimekuwa zikivunjwa na Spika na Naibu wake kila wanapokuwa ndani
ya viti vyao.
Alisisitiza
kuwa hawako tayari na kamwe hawatakuwa tayari kutii mamlaka yoyote
wanayoamini kuwa inawakandamiza na kuwaondolea haki yao, zaidi ya
kupambana.
Kiongozi
huyo alinukuu baadhi ya vifungu vya Kanuni za Bunge alivyosema kuwa
vingetumika kwa kumaliza tatizo la Lissu, aliyemwelezea kuwa alikuwa
sahihi, hata angesimama mara mia moja kwa sababu alikuwa akipinga
upuuzi.
Kuhusu Katiba
Akizungumzia
masuala ya mchakato wa Katiba Mpya, Mbowe alisema kuwa uamuzi
uliotolewa ndani ya Bunge katika hotuba yake ndiyo msimamo wa Chadema,
akatahadharisha kuwa ikiwa Serikali haitakubali kufanya marekebisho
waliyopendekeza, chama hicho kitajitoa.
“Ule ulikuwa
ni msimamo wa Kamati Kuu ya chama chetu na bado tunasisitiza kuwa
wasipokuwa makini tutajitoa. Kama noma na iwe noma, hata kama uchaguzi,
tutashinda kwa nguvu ya Mungu,” alisema na kushangiliwa na umati wa
watu.
Hata hivyo,
alionya kuwa kama Serikali itapuuza ushauri wao, itaisoma namba kwa kuwa
wanajua kinachotaka kufanywa na tayari wameshajipanga kukabiliana
nacho.
Dk Slaa ammwagia sifa Lissu
Kwa upande
wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk Wilbrod Slaa alimwagia sifa Mbunge wa
Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Tundu Lissu, kuwa yeye na wenzake watano waliondolewa kishujaa
na wanatakiwa kusonga mbele zaidi.
CHANZO:Mtandao wa kijamii wa CHADEMA
No comments:
Post a Comment