Manchester United wameondolewa kwenye nafasi ya kwanza ya klabu yenye utajiri na thamani kubwa inayotolewa na jarida la Forbes.
United
wamekuwa wakishika nafasi ya kwanza kila mwaka tangu Forbes walipoanza
kutoa list ya vilabu vye thamani kubwa zaidi duniani mwaka 2004, lakini
mwaka huu wameondolewa kileleni na Real Madrid - klabu ambayo iliitoa
kwenye michuano ya champions league hive karibuni.
Barcelona
wanashika nafasi ya tatu nyuma ya United, Arsenal wapo nafasi ya nne na
mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich wakikamilisha nafasi ya tano.
Real
Madrid wanatajwa kuwa na thamani ya £2.15billion - na kwa namba hizo
klabu hiyo ya Spain inakuwa ndio klabu ya michezo yenye thamani kubwa
zaidi duniani - huku Manchester United wakiwa na thamani ya
£2.07billion.
Kwa upande wa wachezaji wa soka, David Beckham
bado anaongoza kwa utajiri akiwa ameingiza kiasi cha kati ya £33m - £29m
ambazo zimetokana zaidi na mikataba ya kibiashara ya matangazo.
Staa
wa Real Madrid Ronaldo ameingiza kiasi cha (£28.8m) akishika nafasi ya
pili, wakati mwanasoka bora wa dunia Lionel Mess akishika nafasi ya 3
kwa kuingiza jumla ya £26m mwaka jana kwa kupitia mshahara na mikataba
ya kibiashara.
No comments:
Post a Comment