Showing posts with label MAZINGIRA. Show all posts
Showing posts with label MAZINGIRA. Show all posts

Sunday, April 21, 2013

BARAZA LA WAFANYAKAZI MORUWASA LATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI.

Baraza la wafanyakazi MORUWASA lilifanya ziara katika hifadhi ya taifa ya Mikumi baada ya kumaliza kikao chake cha siku mbili katika Hoteli ya Chuo Cha VETA MIkumi.Hii ni rasili mali na hazina kwa Taifa letu,wote tushirikane kulinda na kuhifadhi.

Hapa ni bwawa kati ya mabwawa 3 yaliyochimbwa mbuni mikumi.Wanyama wanaopatikana ni Mamba,Kiboko na ndege maji



Eneo la kuingilia mbugani Mikumi
Pundamilia ambao kitu pekee kwao nikwamba wanasimama kila mmoja akiwa ameelekea upande wake kwa ajili ya usalama

Hawa ni Tembo ambao wanapatikana kwa wingi mbugani Mikumi

Hawa ni nyumbu ambao nao wanapatikana kwa wingi Mikumi.

Hawa ni Twiga ambao kitu pekee kwao ni kuwa wakiwa wanatembea miguu ya upande mmoja inaenda pamoja tofauti na wanyama wengine ambao wanapishanisha miguu.

Huyu ni kiboko aliyemo kwenye mabwawa yaliyochimbwa.

Hawa ni nyati ambao wanasemekana kuwa wanya wakorofi hasa wakimuona mwanadamu.
Mikumi kuna hata uwanja wa ndege,unaweza kutua moja kwa moja na ndege.
Watu husema twiga huwa halali ukweli nikwamba analala kama anavyoonekana lakini hawezi kuinamisha kichwa,analala hivo hivo

Hawa ni swala ambao wanapatikana kwa wingi Mikumi.Kitu cha pekee kwao ni kwamba dume moja unakuta linamiliki kundi kubwa la majike hata kuzidi idadi ya 100.



Thursday, March 21, 2013

KIKAO CHA KAMATI YA MAZINGIRA CHAFANYIKA CHINI YA NAIBU SPIKA UBELGIJI

Mheshimiwa Naibu Spika akiwasilisha taarifa kwenye kikao kinachoendelea Ubelgiji.
 Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jobu Ndugai ameongoza kikao cha kamati ya mazingira na masuala ya jamii ya Mabunge ya Afrika, Carribian na Pacific (ACP) kinachoendelea kufanyika huko Brussels Ubelgiji.
Katika taarifa yake Mh.Ndugai amezungumzia ongezeko kubwa la watu Duniani pamoja na ukosefu wa rasilimali za kuwahudumia.
Picha na Said Yakub

WACHIMBA MADINI NA WAVUVI HARAMU WASABABISHA MAPIGANO MOROGORO

Mkuu wa kituo cha polisi cha kati Morogoro ,Mkuu wa Upelelezi Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA wakiwa eneo la tukio bwawani Mindu
 Katika hali isiyokuwa ya kawaida wavuvi na wachimba madini haramu katika bwawa la Mindu walizua tafrani jana jioni baada ya wachimba madini watatu Andrea Michael, Juma Hassani na Yusuph Abdallah kukamatwa na Maaskari wa kampuni ya Mputa Security wanaolinda bwawa hilo.
Wachimba madini haramu waliokamatwa Mindu kutoka kulia Yusuph Abdallah,Juma Hassan na Andrea Michael
 Askari mmoja alipigwa na wavuvi baada ya kwenda kuwaondoa katika eneo lisiloruhusiwa kuvuliwa samaki, katika kujitetea wavuvi hao waliwapigia simu wenzao ambao walikuja na mapikipiki yapatayo 6 na kila pikipiki ikipakiza watu watatu watatu.
 Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA ilimbidi aende polisi kuchukua maaskari ili kuweza kuimarisha usalama katika bwawa hilo na wakati maaskari wanafika eneo la tukio wavamizi hao walikuwa wameshakimbia lakini walifanikiwa kupata mchimba madini mmoja aitwaye Juma Hassani na kwendanaye kituoni.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita akiongelea swala la kuzima mitambo ya maji na kusababisha mji karibu mzima kukosa maji alisema wamefikia hatua hiyo baada ya maji yaliyokuwa yakiingia kituo cha kutibia maji kuwa machafu sana na yananuka kutokana na mvua kuingiza maji machafu bwawani Mindu.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA akiongea na Chief Kingalu katika eneo la Mindu.

Waandishi wa habari wakiwahoji wachimba madini haramu waliokamatwa bwawani Mindu.


Wednesday, March 20, 2013

MVUA ZASABABISHA MITAMBO YA KUSAFISHA NA KUTIBIA MAJI KUZIMWA MOROGORO

Maji yakiwa yanamwagwa eneo la kutibia maji Mafiga.
 Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha wataalam katika kituo cha kutibu na kusafisha maji Mfiga iliyochini ya Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) kuzima mitambo na kumwaga maji yaliyokuwa yanaingia mitamboni hapo kutoka katika bwawa la Mindu kutokana na maji hayo kuwa machafu sana kwa kujaa tope.
Sampuli ya maji yaliyokuwa yanatoka bwawa la Mindu na kuja sehemu ya kutibia maji Mafiga.
 Hali hii ilizidi zaidi kutokana na mvua iliyonyesha jana jioni hadi usiku iliyoingiza tope jingi sana kwenye mdomo wa bomba la kuchukulia maji katika bwawa la Mindu.Hata hivyo wataalamu hao wamesema watawasha mitambo tu mara hali ya maji itakaporejea katika hali yake ya kawaida.
Kuzimwa kwa mitambo hiyo kumeathiri wakazi wa Maorogoro wanaotegemea chanzo cha Mindu kukosa maji ambao ni zaidi ya 70%.
Bi.Getrude Salema Afisa Uhusiano wa MORUWASA.
 Akiongea na Blogu hii Afisa Uhusiano wa MORUWASA Bi. Getrude Salema amesema hali hii ni changamoto kwa MORUWASA. Hata hivyo amewasihi wakazi wa Morogoro kuwa wawe wavumilivu na kuwa maji yatakayowafikia yatakuwa salama pale tu watakapokuwa wamewasha hiyo mitambo na kuruhusu maji yaanze kuingia na kutibiwa.
Mkondo wa maji ya mvua unaongiza tope bwawa la Mindu.
Blogu hii imefanya ziara hadi Mitambo ya kutibia maji Mafiga, Bwawa la Mindu na Sehemu ambako maji ya mvua yanavuka barabara ya Iringa na kuingia bwawa la Mindu.Kilichoonekana ni uchimbaji wa madini karibu na bwawa,mifugo kutifua ardhi pamoja na kilimo ndo sababu zilizochangia tope kuwa jingi.
Maji ya mvua yakiwa yametuama kando kando ya barabara ya Iringa eneo la Mindu
Hata hivyo,kando kando ya barabara ya Iringa kumeonekana madimbwi mengi ya maji yakiwa yametuama kutokana na makaravati yanayopitisha maji ya mvua kuziba kiasi cha kusababisha maji kukaa kwa muda mrefu na mvua zinaponyesha zinasomba hayo maji hadi bwawa la Mindu.

Wafanyakazi wa MORUWASA wakiwa wameenda kujionea halihalisi ya mikondo inayoingiza maji ya  mvua bwawani.

Friday, March 15, 2013

UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI KANDO MWA MTO RUVU

Wakazi wa kijiji cha Kibangile, Morogoro vijijini wakiwa wanaendelea na uchimbaji haramu wa madini.
 Kumekuwa na kasumba ya wananchi kulalamika kuwa mara mvua hamna, mara jua kali na pia tumekuwa tukiwasikia viongozi na wataalamu mbali mbali wakitueleza kuwa kuna mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni kote, lakini ukija kuchunguza zaidi utangundua kuwa tatizo hilo linaanzia kwa mtu mmoja mmoja hadi kikundi hatimaye kidunia.
Uchimbaji madini kando mwa mto Ruvu
Uharibifu wa mazingira mmojawapo unaoendelea ni uchimbaji haramu wa madini unaoendelea hasa kando kando mwa mito na zaidi mto Ruvu ambao ni mto tegemezi wa vyanzo vya maji kwa mikoa ya Pwani na Dar es salaam ambapo kingo za mto zinaharibiwa na kusababisha maji kusambaa na kuleta mafuriko ikinyesha mvua.
Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu imekuwa na juhudi mbali mbali katika kuhakikisha uchimbaji haramu wa madini hauendelei katika kingo za mito ili kuifanya rasilimali maji inakuwa endelevu.
Uharibifu wa kingo za mto
Mfano ni uchimbaji unaoendelea katika kijiji cha KIBANGILE Wilaya ya Morogoro Vijijini ambako makundi ya watu yamekutwa wakichimba madini, hapa swali ni je,viongozi wa vijiji na kata hawawaoni au nao wanashirikiana nao katika kazi hiyo?

Friday, March 8, 2013

KIKAO CHA BODI YA MAJI CHAFANYIKA MOROGORO

Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Ndg.Washington Mutayoba na kulia ni Katibu wa Bodi Bi.Plaxeda Kalugendo
Kikao cha Bodi ya Maji kimefanyika leo katika ukumbi wa Edema mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe la Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu wakisikiliza kwa makini.
Katika kikao hicho mambo mbali mbali yamejadiliwa na mikakati ya kuboresha utendaji wa Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu imewekwa ili kuifanya Rasilimali Maji iwe endelevu.
Rasilimali Maji katika Wizara ya Maji inasimamiwa na Ofisi za mabonde yapatayo tisa (9) katika nchi nzima.


UHAMASISHAJI JUU UTUNZAJI WA RASILIMALI MAJI BONDE LA WAMI/RUVU

Afisa Maendeleo ya Jamii Bonde la Wami/Ruvu Bi.Nickbar Mwanana Ally akitoa mada wakati wa uelimishaji juu ya zana shirikishi katika usimamizi wa pamoja wa rasilimali maji katika Shule ya Msingi Kisemu-Mtamba Morogoro vijijini.
Katika kuhakikisha rasilimali maji inakuwa endelevu,Bonde la Wami/Ruvu linafanya jitihada za kuwahamasisha na kuwaelimisha wanchi wa Mikoa ya Dodoma,Morogoro,Pwani,Tanga na Dar es salaam juu ya utunzaji wa rasilimali hiyo.
Wakazi wa Morogoro vijijini kutoka vijiji 13 wakishiriki mafunzo katika shule ya msingi Kisemu-Mtamba

Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu inaendesha mpango wa ZANA SHIRIKISHI KATIKA USIMAMIZI WA PAMOJA WA RASILIMALI MAJI.Mpango huu unaendeshwa katika vijiji vyote na wananchi wanahamasishwa kushiriki katika shughuli za utunzaji vyanzo vya maji.
Miti jamii ya Misederea ambayo wakazi wengi wa Morogoro vijijini na Mvomero wameipanda kwa wingi karibu na vyanzo vya maji bila kuelimishwa wapi mahali bora pakupanda.Ukweli nikwamba miti hii ni hatari kuipanda karibu na vyanzo vya maji maana inanyonya maji kwa kasi sana.
Maofisa wa ofisi za Bonde la Wami/Ruvu wakichota maji katika moja ya chanzo cha maji Morogoro vijijini.Vyanzo vya maji vikitunza vizuri ni hazina ya sasa na kwa kizazi kijacho.

Monday, March 4, 2013

MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA NA AFYA MOROGORO



Mtafiti mkuu wa mradi Profesa Jamidu Katima akisaini kitabu cha wageni wakati wa utambulisho wa mradi.
Manispaa ya Morogoro imepata bahati ya kujengewa mradi wa uondoshaji wa majitaka na uhifadhi wa mazingira unaojengwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha Uhandisi (COET) unaofadhiliwa na COSTECH ambao ni mradi wenye thamani ya zaidi ya Milioni 200 unaojengwa Mafisa katika mabwawa ya majitaka ya MORUWASA.

Bwawa litakalo kuwa linatumika kutibu majitaka.
Mradi huo ujulikanao kama Constructed wetlands and fish ponds.Katika mradi huo ambao malengo yake ni utafiti juu ya matumizi ya majitaka baada ya kutibiwa na kujenga mabwawa ambayo ni ya bei nafuu.
Bwawa la kufugia samaki katika mradi huu.
Katika mradi huo utahusisha ujenzi wa mabwawa ya samaki na kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kuthibitisha kama majitaka hayo baada ya kutibiwa yanaweza kutumika kwa ufugaji wa samaki na umwagiliaji.

Utafiti juu ya kilimo gani kitafaa kulimia kutumia maji hayo,hapa ni Mpunga,nyanya na Chinese.
 Akiongelea juu ya baadhi ya faida za mradi huo ,mtafiti mkuu wa mradi huo profesa Jamidu Katima alisema kuwa ni gharama ndogo za ujenzi,hupunguza adha ya harufu mbaya,maji yake yanaweza kutumika katika kujikwamua kiuchumi.

Friday, March 1, 2013

MSAKO MKALI WA UCHIMBAJI WA MADINI KANDO MWA BWAWA LA MINDU.

Ndg.Christopha Evarist Bengu aliyekamatwa akichimba madini kando mwa Bwawa la Mindu.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) inaendelea na zoezi la kuhifadhi mazingira katika vyanzo vyake vya maji kwa wakazi wa Morogoro.Katika kuhakikisha hilo leo Maaskari wanaolinda Bwawa la Mindu wameweza kuwakimbiza watu zaidi ya kumi (10) waliokuwa wanachimba madini lakini wakafanikiwa kumkamata mchimbaji mmoja.

Ndg.Christopha Evarist Bengu akiwa chini ya ulinzi
Akiongea na Blogu hii Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita amesema mtuhumiwa huyo aitwaye Ndg.Christopha Evaristi Bengu anapelekwa Polisi kwa kuweza kupelekwa Mahakamani.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita.
Ikumbukwe kwamba wakazi wa Morogoro mpaka sasa wana uhaba mkubwa wa maji kutokana na ukame unaosababishwa na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wakazi wa Morogoro.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...