Tuesday, November 6, 2012

MATUNDA.
Morogoro inasifika kwa kuwa na matunda aina mbali mbali ya kutosha ambayo yanapatikana maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro.
Changamoto kubwa ninayoiona hapa ni utunzaji wa matunda hayo yanayoletwa mjini.Yanamwagwa tu chini bila kujali usalama wake swala ambalo linaweza kuleta madhara kiafya kwa walaji.Wafanya biashara wa matunda wawe wanafatiliwa kwa ukaribu ili kuweza kuwadhibiti kutoharibu ubora wa matuda hayo.Wafanyabiashara hawa wamekutwa wamemwaga matunda chini eneo la Sume Mwembesongo.

1 comment:

  1. Kwa mara nyingine msimu wa matunda Morogoro umewadia,matunda yamefurika katika soko la matunda Mawenziambako matunda kutoka milimani hushushwa na wananchi kwenda kununua.
    Wito wangu kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro na maeneo ya jirani wanatakiwa kuwa makini sana katika kutumia matunda haya kwa kuzingatia kanuni za afya.Kipindi hiki ndicho kipindi hatari kwa magonjwa ya milipuko kama kipindu pindu.
    Pili nawaomba wale wote wanaofanya biashara ya matunda kuyahifadhi katika mazingira ya kiusafi ili kulinda afya za wateja wao.
    Tatu naiomba halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kupitia idara ya afya kufatilia kwa ukaribu zaidi uuzaji wa matunda ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka magonjwa ya milipuko.
    NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WA 2013.

    ReplyDelete

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...