Tuesday, June 18, 2013

ZIARA YA WAKALI WA KILI MUSIC AWARDS 2013 MKOANI DODOMA.

Ziara za wakali wa Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka 2013, inaanza rasmi kutikisa Mjini Dodoma Jumamosi hii, Tarehe 22 katika viwanja vya Jamhuri ambapo wakazi woote wa Dom watapata nafasi pekee ya kuwaona mastaa waliofanya vyema kwa mwaka huu katika jukwaa moja wakitoa burudani isiyopimika.

Kwenye lineup ya Dodoma, wamo wakali kama vile Binti Comando a.k.a Anaconda ama Lady Jay Dee, Ommy Dimpoz, Ally Kiba, ROMA, Proffesa Jay, Kala Jeremiah, Ben Pol pamoja na Linex

Kili Music Awards kwa mwaka huu inakwenda kwa Slogan ya Kikwetu kwetu kwani burudani itakayokuwa ikitolewa ni kutoka kwa wasanii wa nyumbani,wakitupa burudani za nyumbani na katika viwanja vya nyumbani.

Mchongo utaanza saa 10 jioni kwa kiingilio cha shilingi elfu mbili na mia tano tu (2500/=), na kuifanya iwe poa zaidi, utatuzwa bia moja ya kilimanjaro mlangoni.

Wakazi wote wa Kanda za kati Dodoma mkae mkao wa kula,sebene la nguvu linawajia.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...