Thursday, June 6, 2013

JIJI LA MWANZA LAENDELEA KUSHIKILIA TAJI LA USAFI TAIFA.

Kwa mara ya nane mfululizo jiji la Mwanza limeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa jiji linaloongoza kwa Usafi Tanzania.Ushindi huo umetangazwa jana katika kilele cha siku ya mazingira kitaifa sherehe zilizofanyika Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa.Akiongea na blogu hii Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula  amesema kuwa Jiji lake liko kwenye mpango wa kushindana kimataifa kwa usafi.
Hongera sana Mwanza na majiji mengine yanatakiwa kuiga mfano huo ili nayo yaweze kutwaa taji hilo.
Miongoni mwa mitaa ya Jiji la Mwanza.




No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...