Monday, June 3, 2013

SASA "SHOW" YA LADY JAYDEE NI JUNE 14.

Msanii muziki Lady Jaydee  ametangaza rasmi tarehe yake ya kufanya show ya miaka13 toka ameanza kufanya muziki kuwa ni siku ya Ijumaa ya Tarehe 14 mwezi Juni, baada ya kuaihirisha show yake kufuatia kifo cha Msanii Albert Mangwea kilichotokea siku ya tarehe 28 huko Afrika Kusini.
 
Lady Jaydee amesema sababu ya kuchagua siku hiyo ni kwamba siku ya Tarehe 13 atakwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili na siku inayofuta itakuwa show ya Miaka kumi na tatu (13) na tarehe 15 atasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
 
Lady Jay Dee  ametumia akaunti yake ya twitter kuiweka wazi tarehe ya show yake alipokua akijibu swali la fan wake ambae atasherehekea siku moja ya kuzaliwa na msanii huyo (June 15).

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...