Thursday, June 13, 2013

WATOTO 93,000 WAMEUAWA SYRIA.

Makaburi ya watu waliouawa nchini Syria.
Umoja wa Mataifa umesema takriban watoto elfu tisini na tatu wameuawa nchini Syria tangu kuanza kwa mapigano nchini humo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya elfu thelathini, tangu umoja huo ulipotoa takwimu zake Januari mwaka huu.
Ripoti hiyo imesema kuwa watu elfu tano hufa nchini Syria kila mwezi tangu Julai mwaka uliopita
Hata hivyo takwimu hizo huenda sio idadi kamili na Umoja wa Mataifa umesema huenda idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi, kwa kuwa vifo vingi havijaripotiwa.
Asilimia themanini ya waliouawa ni wanaume, lakini Umoja huo umeongeza kusema kuwa tayari umethibitisha kutokea kwa vifo vya zaidi ya watoto elfu moja mia saba ambao wako chini ya umri wa miaka kumi.
Vile vile, kuna ripoti kuwa watoto wengine waliteswa kabla ya kuuawa kinyama.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadam Navi Pilllay, amesema wamepokea ripoti ya kutokea kwa mauaji ya familia nyingi wakiwa na watoto wao, ishara kuwa vita vinavyoendelea nchini Syria vimegeuka kuwa janga kuu huku maelfu ya watu wakiendelea kuuawa kila siku.

Source: BBC.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...