Wednesday, June 19, 2013

SUA WAKABIDHI MRADI WA ZAIDI YA MIL.100 KWA MORUWASA.


Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) leo hii kimekabidhi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira (MORUWASA) mradi wa Majitaka wa zaidi ya Tsh. Milioni 100 uliojengwa na Chuo hicho wenye umbali wa zaidi ya Kilometa 1. Mtandao huo unatoka katika Hosteli za wanachuo zilizo eneo la Misufini karibu kabisa na Makao makuu ya chuo hicho.Hosteli hizo zina uwezo wa kuhudumia wanachuo 1350.
Ndg.Hezron K.Sanga- Afisa Mipango Mkuu SUA.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo,Afisa Mipango Mkuu wa Chuo hicho Ndg.Hezron K.Sanga amesema kuwa mradi huo uligharimu Tsh. Milioni 104 mpaka kukamilika.
Ndg.D.M.T. Komba- Meneja Miliki SUA
Makabidhiano hayo yalifanyika katika Hosteli hizo kati ya Uongozi wa SUA uliowakilishwa na Ndg.Hezron K.Sanga (Afisa Mipango Mkuu-SUA) na Ndg.D.M.T. Komba (Meneja Miliki- SUA) na kwa upande wa MORUWASA iliyowakilishwa na Eng.Halima Mbiru (Meneja Ufundi-MORUWASA), Eng.Sigsbert Ishengoma (Mkuu wa Kitengo cha Majitaka na Mazingira -MORUWASA), Ndg.Rashid N.Bumarwa (Afisa Afya na Mazingira - MORUWASA), Bi.Getrude Salema (Afisa Mahusiano- MORUWASA), na Ndg.Festo Mkoma (Msimamizi wa Mtandao wa majitaka -MORUWASA).
Eng.Halima Mbiru - Meneja Ufundi MORUWASA.
Kukamilika kwa mradi huo kumetatua tatizo kubwa lililokuwa linawakumba wakazi wa kata ya Mafiga hasa mitaa ya Misufini,Kidondolo na maeneo yote yaliyokaribu na eneo hilo.
Eng.Sigsbert Ishengoma - Mkuu wa kitengo cha majitaka na mazingira MORUWASA.






Hosteli mpya za SUA.


Hosteli mpya za SUA.






No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...