Saturday, June 1, 2013

DR.SLAA NA HECHE WAFUNIKA MOROGORO.


Katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa akiambatana na Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA Ndg.John Heche leo wamehutubia umati mkubwa wa maelfu ya watu waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja wa ndege/Saba saba.

Akiuhutubia umati huo zaidi zaidi ameongelea swala la amani ya nchi yetu ya Tanzania.Akiongea Dr. Slaa amesema kuhubiri majukwaani,makanisani,misikitini,mikutanoni,vikaoni,bungeni au mahala popote kuwa tuilinde amani yetu ya Tanzania na kumuomba mwenyezi mungu ni uongo mtupu ikiwa amani hiyo hujaitengeneza na kuisababisha iwepo.

Akiendelea kuhutubia amesema mfanyakazi,mama lishe/baba lishe, machinga,mwendesha boda boda,polisi au mtu yeyote hawezi kuwa na amani wakati hana uhakika na maisha yake kwa umaskini.

Dr.Slaa akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo.


Watu wakiwa wanamsikiliza Dr.Slaa juu ghorofani kwenye jengo la CCM Mkoa wa Morogoro.

Ghari la matangazo la CHADEMA.


Mwanachama wa CUF akiwa anamuuliza maswali Dr.Slaa katika  mkutano huo.

Wananchi wakilisindikiza gari la Dr.Slaa.

Askari polisi wakilisindikiza gari la Dr.Slaa.


Wakazi wa Morogoro wakilejea makwao baada ya mkutano.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...